Uswahilini kuna mambo! Wanawake wawili waliofahamika kwa jina moja
moja la Asha na Mariamu wakazi wa Gongo la Mboto, jijini Dar hivi
karibuni walizichapa mchana kweupe wakiwa harusini kwa ajili ya
kumgombea mwanaume.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio zima
ambapo wawili hao walikuwa miongoni mwa washiriki wa sherehe ya harusi
hiyo na wote wakiwa wamevaa madira.
Asha alionekana akiwa karibu na mwanaume aliyesababisha tafrani hiyo ambaye hata hivyo hakufahamika jina lake mara moja.
Ilidaiwa kuwa mwanaume aliyegombaniwa, awali aliwahi kuwa na uhusiano
wa kimapenzi na Mariamu kabla ya kuachana na kuanzisha urafiki na Asha.
Wakiwa wanaendelea kucheza muziki, walionekana kufanyiana vituko kwa
ishara huku kila mmoja akijiona ndiye anayefaa, hatimaye uzalendo
ulimshinda Asha aliyemfuata na kumvamia Mariamu na kuanza kuzichapa,
wakang’atana na kuvuana nguo hadharani huku watu wakishangilia.
Mtiti
ulikuwa mkali hali iliyosababisha Mariamu abakie na nguo za ndani pekee
huku Asha akidai kuwa mwenzake huyo alikuwa akimcheka kwa muda mrefu.
“Siwezi kukubali hata kidogo kwa sababu nilikuwa nacheza yeye akasema
eti nilikuwa namcheka, kwa lipi, kama huyo mwanaume hapa kwangu ni kama
msikiti, asipokuja kusali atakuja maiti,” alisikika akitamba Mariamu.
Baada ya vurumai hiyo, Asha alitokomea kusikojulikana akiwa na mwanaume huyo huku hasimu wake akiondoka na kundi la marafiki zake kuelekea nyumba anayoishi adui yake kwa maelezo kuwa watamsubiri hadi atakaporejea ili wazichape upya.
Baada ya vurumai hiyo, Asha alitokomea kusikojulikana akiwa na mwanaume huyo huku hasimu wake akiondoka na kundi la marafiki zake kuelekea nyumba anayoishi adui yake kwa maelezo kuwa watamsubiri hadi atakaporejea ili wazichape upya.
CHANZO NI GPL
Ama kweli uswahilini kuna vituko
ReplyDelete