
IMEPITA miezi minne tangu msanii mkongwe Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ aingie kwenye ndoa, juzikati amefunguka kwamba amegundua ndoa ni tamu na anajiuliza kwa nini hakulijua hilo mapema.
Akistorisha na gazeti hili, Natasha alisema baada ya kuingia kwenye ndoa amejikuta akifurahia maisha tofauti na yale aliyokuwa akiishi wakati wa ubachela.
“Nafurahia ndoa kwa sababu tuko wawili, nikisikitishwa na jambo napata faraja kutoka kwake. Nikitaka kwenda mbali naomba ruhusa kwa mume wangu, hilo pia linanipa furaha,” alisema Natasha.
CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment