Waziri Mkuu wa wa Latvia, Valdis Dombrovskis,
amejiuzulu kufuatia kuporomoka kwa jengo moja nchini humo, Alhamisi
iliyopita na kusababisha watu wapatao hamsini kuuawa.
Bwana Dombrovskis amesema amekubali kuwajibika
kisiasa kutokana na mkasa huo ambapo paa ya duka moja kubwa la bidhaa
katika mji mkuu, Riga, lilipinda na kuporomoka.
Polisi wameanzisha uchunguzi wa kihalifu kubaini
kama taratibu za ujenzi wa jengo hilo zilizingatiwa au la; bustani
ilikuwa ikijengwa juu ya paa la jengo hilo la maduka wakati ajali hiyo
ikitokea.
Latvia imekuwa na siku tatu za maombolezo
kuwakumbuka waathirika wa janga hilo, ambalo ni baya kuwahi kutokea
nchini Latvia, tangu nchi hiyo ijipatie uhuru wake mwaka 1981.
Kujiuzulu kwa Bwana Dombrovskis, ambaye ameiongoza Latvia katika kipindi cha mgogoro wa kiuchumi, kumekuja wiki kadhaa kabla ya nchi hiyo kujiunga na umoja wa Ulaya.
Kujiuzulu kwa Bwana Dombrovskis, ambaye ameiongoza Latvia katika kipindi cha mgogoro wa kiuchumi, kumekuja wiki kadhaa kabla ya nchi hiyo kujiunga na umoja wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment