Baada ya kusema hayo nianze kusema kwamba naipongeza serikali kwa
kuanza kuchukua hatua baada ya nchi za Rwanda, Kenya na Uganda
kutoihusisha nchi yetu katika mambo yanayohusu Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC), ikiwa ni pamoja na kutohudhuria mikutano ya jumuiya
hiyo yenye ajenda ambazo nchi hizo tatu zimekwishaweka msimamo wa peke
yao.
Kutoka kushoto ni Paul Kagame, Yoweri Mseveni na Uhuru Kenyatta.
Nchi za Rwanda, Uganda na Kenya zimeanzisha ushirikiano wa pamoja katika maeneo ya miundombinu, biashara na viza ya pamoja na mara nyingi viongozi wakuu wa nchi hizo wamekuwa wakifanya mikutano bila kuihusisha Tanzania na Burundi, ni dhahiri kwamba hawatutaki.
Serikali hivi karibuni kupitia kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ilitoa ufafanuzi bungeni kuhusu kutengwa huko baada ya wabunge kutaka ieleze msimamo wake kuhusu suala hilo, hasa baada ya kuonekana dhahiri kwamba nchi yetu inatengwa.
Waziri Sitta alisema: “Si kwamba serikali imekaa kimya, kuna mambo mengine yanaendelea. Tumeanza kuchukua hatua kuonyesha kuwa hatuwezi kuendelea na hali hii inayofanana na mchezo wa kuigiza.”
Sitta alisema kuwa hivi sasa Serikali haitashiriki katika mikutano ya jumuiya hiyo ambayo ajenda zake zinahusu mambo ambayo nchi hizo tatu zimekubaliana peke yao. “Kuna mkutano jijini Nairobi unaowahusisha mawaziri wa mambo ya nje, mamlaka kuu imeamua kwamba waziri wetu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe asihudhurie,” alisema Sitta.
Ndugu zangu ukweli ni kwamba kama tunazungumza sera ya mambo ya nje na wenzetu wanataka kuunda shirikisho bila kutushirikisha, haitakuwa na maana sisi kwenda kukaa katika vikao ambavyo hayo yanayozungumzwa wao tayari wamekwishayawekea msimamo.
Nakubaliana na serikali kwamba ichukue hatua na isishiriki katika vikao vyao, kama wao wamekubaliana, basi haipo sababu ya sisi kwenda kwenye vikao vyao.
Nilifarijika sana kusikia kuwa serikali ilimuagiza Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Abdullah Abdullah kutohudhuria kikao chao cha hivi karibuni, kwa maelezo kuwa ajenda za mkutano huo zilihusu mambo ambayo tayari nchi hizo zimekubaliana.
Kwa kuwa Waziri Sitta alisema mpaka sasa Tanzania inatafuta ufafanuzi wa suala hilo Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwamba baada ya wiki mbili yatatolewa majibu na Tanzania itachukua hatua, naomba sana iwe kama serikali ilivyosema.
Binafsi nalaani nchi hizo kuanzisha jumuiya ndani ya jumuiya na napendekeza Tanzania iunde jumuiya mpya itakayozihusisha nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Burundi.
Tunajua kwa nini nchi zile tatu zinatukataa, jibu ni rahisi sana ni kwa sababu Tanzania tumekubali kupeleka majeshi yetu Congo kupambana na waasi wa M23!
Lakini nitapenda serikali iseme msimamo wa nchi yetu kiuchumi iwapo jumuiya hiyo itavunjika, kwani kuna madai kuwa tayari Kenya imekubaliana na Ethiopia na Sudan kwa ajili ya kutumia nchi hizo kibiashara.
Jambo ambalo nina uhakika nalo ni kwamba Tanzania ina utajiri mkubwa sana wa miundominu ya bahari kwa sababu tuna bandari kubwa tatu katika Bahari ya Hindi, ambazo ni Tanga, Dar es Salaam na Mtwara na katika Ziwa Tanganyika pale Kigoma, hivyo tukishirikiana na Congo DR na Burudi, sidhani kama tutakuwa na shida.
Hakika mimi nahimiza Tanzania tujikite zaidi katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) huku tukijiuliza ni kwa nini inatengwa?
Nionavyo mimi ni kwamba jumuiya ya sasa bado haijawa na nguvu ya wananchi na inaendeshwa na mawazo ya viongozi jambo ambalo linatishia uhai wake kama iliyokufa mwaka 1977. Kinachojitokeza sasa ni kushindwa kujifunza kupitia udhaifu wa jumuiya iliyovunjika ambayo ilitokana na kuachwa iendeshwe na viongozi na baada ya kutokea mgongano wa mawazo ukasababisha jumuiya kusambaratika.
Nasema msimamo wa serikali katika suala la jumuiya ni sahihi na ndiyo ilikuwa shaka ya Watanzania tangu nchi iliposaini kujiunga na jumuiya hiyo.
Jumuiya ya sasa ni tofauti na iliyovunjika awali, kwani hii inaonekana kuwa baadhi ya nchi ziko kwa ajili ya masilahi binafsi zikitumia mgongo wa jumuiya kujipatia ardhi na kutafuta soko ndani ya eneo la nchi wanachama wa Jumuiya.
Umoja wa Ulaya (EU) nguvu yake ya uchumi ni asilimia 23, lakini nchi 54 za Afrika nguvu yake ya uchumi ni asilimia 2.5, hivyo kuungana kwa nchi tano ambazo zinatoka kwenye kundi dhaifu hakusadii lolote Tanzania.
Hata ukiangalia sasa kutokana na mtangamano huu, asilimia 60 ya bidhaa zilizopo nchini zinatoka Kenya wakati sisi tunauza kwao malighafi.
Tanzania inaweza kuja na njia bora na salama ya kuinua uchumi wa nchi, ikiwa ni pamoja na kuangalia jinsi ya kuthaminisha bidhaa na kuondokana na kuuza nje ya nchi malighafi.
China wanauza bidhaa dunia nzima kwani wameungana na nani?
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment