SPIKA wa Bunge Anne Makinda amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki, kuchunga kauli zake anazotoa nje ya Bunge, kwani zinaingiliana na utendaji kazi wa mhimili huo wa dola.
WAZIRI KAGASHEKI |
Onyo hilo la Spika amelitoa baada ya Mbunge wa Sikonge, Saidi Nkumba (CCM), kuomba mwongozo wa Spika na kuelezea kitendo cha Balozi Kagasheki kutoa matamko mbalimbali nje ya Bunge, kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili iliyositishwa baada ya wabunge
kulalamika, kuna ukiukwaji wa haki za binadamu.
“Mheshimiwa Spika naomba mwongozo wako, kama jambo hili linaruhusiwa au haliruhusiwi kwa mujibu wa kanuni …ni juzi tu waheshimiwa wabunge na Bunge lako tukufu limejadili kwa kina suala la dharura juu ya maonevu ambayo wamefanyiwa wananchi wetu maeneo mbalimbali wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
“Lakini siku chache baada ya kujadili jambo hilo, Waziri Kagasheki ameonekana na akinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba wabunge wanasemasema tu ndani ya Bunge bila kujali rasilimali za taifa,” alisema Nkumba.
Kwa mujibu wa Nkumba, Kagasheki amenukuliwa na vyombo vya habari, akidai hatishwi na maelezo ya wabunge ya kumtaka ajiuzulu na kwamba hatang’oka madarakani mpaka Rais Jakaya Kikwete aliyemteua, atakapomtaka afanye hivyo.
Alisema yeye mwenyewe, ndiye aliyetoa kauli ya kusitisha operesheni tokomeza bungeni, na kitendo cha kuwakamata Wachina ni kazi ya Serikali ya kila siku, ambayo inaweza kuendelea bila operesheni.
Alimtaka Spika afafanue kuhusu kauli ya Kagasheki, ambayo ameitoa ndani ya Bunge na kuipeleka nje, ilhali suala hilo bado linafanyiwa kazi.
Akitoa mwongozo, Spika alisema anadhani kuna matumizi mabaya ya midomo kwa baadhi ya wabunge na watendaji nchini.
“Nasema tukishakubaliana hapa, halafu unakwenda kusemasema huko nje ni kuwasha moto, pale ambapo moto tayari unawaka, matamko ambayo si mazuri, tuyaepuke…”alisema Spika Makinda.
Akitoa mwongozo, Spika alisema anadhani kuna matumizi mabaya ya midomo kwa baadhi ya wabunge na watendaji nchini.
“Nasema tukishakubaliana hapa, halafu unakwenda kusemasema huko nje ni kuwasha moto, pale ambapo moto tayari unawaka, matamko ambayo si mazuri, tuyaepuke…”alisema Spika Makinda.
Suala la ujangili na migogoro ya wakulima na wafugaji, liliibua mjadala mkubwa bungeni wiki ilyopita na kusababisha Serikali kusitisha operesheni hiyo ili kufanya tathmini ya athari hasi.
CHANZO HABARI LEO
No comments:
Post a Comment