EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, December 18, 2013

Air Tanzania yarudisha safari za ndege za kwenda Burundi

 Meneja Rasilimali watu kutoka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Eliezer Mwasele, akishuka kutoka ndani ya ndege mara baada ya ndege ya Air Tanzania kutua wakati wa uzinduzi wa safari za kwenda Bujumbura- Burundi. Nyuma yake ni aliekuwa Balozi wa Tanzania Burundi, Francis Mndolwa.
 Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi (kushoto) akiwa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa (wa pili kushoto) mara baada ya kupokea ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania, Air Tanzania, iliyoanza sarai za kwenda Bujumbura mwishoni mwa wiki. Wengine mbele ni baadhi ya mawaziri wa serikali ya Burundi.
 Baadhi ya abiria wakipanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania –Air Tanzania- kabla ya kuanza safari ya kuelekea Bujumbura –Burundi, wakati wa uzinduzi wa safari hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya viongozi wakisindikiza abiria walioshuka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania –Air Tanzania- mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bujumbura- Burundi kama ishara ya uzinduzi rasmi wa safari hizo. Kutoka kushoto ni Waziri wa Burundi wa Afrika Mashariki, Bi Nziyemana Leontine akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa
 ========   ========   ==========
Air Tanzania yarudisha safari za ndege za kwenda Burundi
·       Waanza safari za kwenda Mbeya
·       Warejesha safari za Mwanza

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL) limezindua rasmi huduma za usafiri wa anga kutoka Dar es Salaam kuelekea Bujumbura, Burundi kwa kupitia mkoani Kigoma, safari hizo zitafanyika mara tatu kwa wiki yaani Jumatano, Ijumaa na Jumapili.
Hatua hiyo imekuja baada ya hali ya amani kutengamaa katika nchi hiyo ya Burundi ambayo ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuilazimu Tanzania kusitisha huduma hizo kwa muda wa miaka 20.
Wakati huo huo, ATCL pia imeanza safari za Dar es Salaam kwenda Mbeya, safari hizo zitafanyika mara nne kwa wiki yaani Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili. imerejesha safari za Dar es Salaam – Mwanza kila siku, safari  zilizoanza rasmi Jumapili iliyopita. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Bujumbura Burundi katika uzinduzi wa huduma hizo juzi, Meneja Rasilimali watu wa Shirika hilo la ndege, Ndugu Eliezer Mwasele, alisema uzinduzi wa safari hizo utakuwa ni njia mojawapo ya kuchochea maendeleo ya uchumi kwa nchi zote mbili.
Alisema kutokana na hali hiyo Watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika nchi hiyo ya Burundi, kwani asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa nchi za Kongo na Burundi wanatarajiwa kuanza kutumia usafiri huo kwa wingi.
Akizungumzia hatua hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi, alisema kuanza kwa safari hizo ilikuwa ni ndoto ya siku nyingi ambayo aliipigania na kutamani kuona wananchi wa pande zote mbili wananufaika kwa pamoja.
“Tumefurahi sana kwa kutimiza ndoto hii leo (juzi), kwa sababu sasa uhusiano kati ya nchi hizi mbili unazidi kuimarika hasa ukizingatia tunategemena kibiashara kulingana na fursa zilizopo.
Kwa upande wake, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa, alisema kwa kuwa ATCL imefunga mkanda na kuanzisha tena safari hizo, ni vyema ikazingatia muda na kuhakikisha huduma stahiki zinatolewa ili kukuza shirika hilo.
Naye Waziri wa Burundi katika Bunge la Afrika Mashariki, Nziyemana Leontine alisema, “kuanzishwa kwa Air Tanzania kuja Burundi, kutasaidia wananchi wa Burundi, hususani wafanyabiashara kwani walikuwa wanaunganisha ndege kupitia nchi nyingine, lakini sasa hivi wananchi watakuja moja kwa moja. Tunashukuru sana,” alisema.
Naye mmoja wa abiria kutoka Burundi waliopanda ndege hiyo, Dk. Owera Kodime, alisema, kuanzishwa kwa safari hizo kutawapunguzia sana gharama za usafiri wananchi wa Burundi, kwa sababu Tanzania imepunguza gharama kuliko mashirika mengine.
“Tulikuwa tukitumia muda mrefu sana kuzunguka lakini sasa tutaweza kuja moja kwa moja Dar es Salaam, ni hatua nzuri ambayo imetuletea faraja sana Warundi,” alisema.
Kwa upande wa abiria kutoka Tanzania, Joseph Kisaro, alisema, “ Muda mrefu sana kulikuwa hakuna huduma, tangu mwaka 1993 huduma zilikatatika, lakini uongozi wa Tanzania umefanya juhudi baada ya mapigano kuisha. “Tunashukuru ubalozi ulioteuliwa mwaka 2003 kwani ulianza harakati haraka za kurudisha huduma hizi ambazo sasa tumefanikiwa.
“Tunaomba uongozi wa ATCL uangalie pia kuwa na safari za kuelekea Kongo mashariki kwa sababu kuna abiria wengi sana ambao ni wafanyabiashara wanaokuja Tanzania,” alisema

WAZIRI WA ARDHI, MAKAZI NA NISHATI MHE. RAMADHAN SHAABAN AFUNGUA JENGO LA OFISI YA KITENGO SHIRIKISHI CHA AFYA YA MAMA NA WATOTO ZANZIBAR

 Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Mhe. Ramadhan Shaaban akikata utepe wakati akifungu Jengo la Ofisi ya Kitengo Shirikishi cha Afya ya mama na mtoto kiliopo Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Mdhamini wa kitengo Shirikishi Afya ya Mzazi na Mtoto Dkt. Ali Omar Ali akimfahamisha kitu Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Mhe. Ramadhan Shaaban alipokua akikagua jengo hilo mara baada ya kulifungua huko Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Baadhi ya wageni walikwa waliohururia katika ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Kitengo Shirikishi cha Afya ya mama na mtoto huko Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  Waziri wa Afya Juma Duni Haji akimkaribisha mgeni rasmin Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Mhe. Ramadhan Shaaban azungumze na wageni waalikwa katika sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Kitengo Shirikishi cha Afya ya mama na mtoto huko Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Mhe. Ramadhan Shaaban akiwahutubia wageni walikwa katika ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Kitengo Shirikishi cha Afya ya mama na mtoto liliopo Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate