Na Hamida Hassan
Katibu wa chama cha waigizaji Bishop Hiluka amemzika baba yake leo aliyefariki Dunia Desemba 8 mwaka huu katika hospitali ya Hindumandal baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
Mazishi hayo yamefanyika kwenye makaburi ya Tegeta jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wasanii kibao wakiongozwa na Rais wa Taff Simon Mwakifamba na makamu wake mzee Ling’ande.
Wasanii waliofika msibani hapo walijitoa kwa hali na mali kuhakikisha wanamzikia katibu wao.
Baadhi ya wasanii waliofika ni pamoja na Vanita Omari, Elizabeth Kijumba ‘Nikita’, Mike Sangu, Deogratius Shija, John Lisa,Mzee Bawji, Kelvin, Rado, Paul… na wengine wengi
No comments:
Post a Comment