STAA
wa filamu Bongo anayetamba na ngoma yake ya Summer Holiday amesema kuwa
kutokana na mahaba mazito anayopatiwa na mwandani wake Joe Kariuki
ambaye ni Meneja wake hafikirii kumuacha kamwe.
Akipiga
stori na paparazi wetu alisema, tangu aanze uhusiano na pedeshee huyo
anayemiliki studio ya Candy n’ Candy nchini Kenya, amekuwa akijiona
mwenye fahari kubwa kwenye sayari ya mapenzi kutokana na upendo
anaomuonesha na kumfanya asiwaze kumpotezea kamwe.
“Kusema kweli huyu kaka kanikoleza jamani japo watu watachonga mengi
lakini abadani sitosikiliza maneno yao, kwa kuwa awali sikuwa na
uhusiano naye ila porojo za watu zilipelekea kuchukua maamuzi hayo
natamani niamie Kenya ili tuwe karibu wakati wote,”alisema Baby Madaha.
Aliongeza kuwa kikubwa kilichompelekea kuwa naye ni kutokana na
upendo wake wa kweli alionao kwake siyo kutokana na suala la mkwanja
kama wengi wanavyodhani.
- CREDIT: GPL
No comments:
Post a Comment