
Aidha Manji ametangaza mkutano mkuu wa wanachama Januari 19,2013 ambapo wanachama watapata fursa ya kupitia mapato na matumizi, na ajenda zingine mbalimbali ambazo zitajadiliwa katika mkutano huo.
Kikao cha kamati ya utendaji kilichoketi mwishoni mwa wiki kimemteua Bw.Seif Ahmed "Magari" kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa na kutokana na nafasi hiyo pia ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji wa klabu ya Yanga.
Katika mkutano na wandishi wa habari makao makuu ya klabu Manji ametangaza rasmi kutogombea tena uenyekiti katika uchanguzi mkuu ujao, hili nimeliamua mwenyewe binafsi bila shinikizo na kikubwa nimefuata demokrasia.
Nina miezi saba kabla ya uchanguzi mkuu mwakani hivyo sasa ninajitahid kukamlisha shughuli zote ambazo nilianza kuzifanya ndani ya Yanga nikiwa kama mwenyekiti ili uongozi mpya utakaoingia uweze kuendeleza mipango ya kuifanya Yanga iwe klabu bora Tanzania.
CHANZO NI YANGA
No comments:
Post a Comment