Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji
wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua
akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.
Emmanuel Okwi akiweka alama ya Dole Gumba mbele ya Mjumbe wa Kamati ya
Mashindao Musa Katabaro (kushoto) wakati akisaini mkataba wa kuichezea
Yanga mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016. kulia ni mwanasheria/meneja
wa Okwi Bw. Edgar Agaba
Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki
wengi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika
klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa
2015/2016.
Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania
limefungwa usiku wa kuamkia jana Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa
kihistoria klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa
ni pamoja na kupata hati ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.
Usajili
wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji
watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna
Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu
Uongozi
wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano
wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la
usajili.
Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi
karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma Kaseja
ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka
timu ya Ruvu Shooting.
Baraka Kizuguto
Afisa Habari – Young Africans SC
Disemba 15, 2013.
(Picha na
Yanga).
No comments:
Post a Comment