STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na kusema kuwa anahitaji mume anayemzidi umri kwa miaka kumi.

“Ninamtaka mwanaume anayenizidi miaka kumi kwani kwa sasa nina miaka
31 japokuwa kwa sasa nafanya kazi kwanza ili nirudi kwenye levo yangu na
nitakuwa juu zaidi ya zamani kwa sababu najitambua japokuwa nina hamu
sana ya mtoto lakini yote namwachia Mungu.

Aidha, Ray C alisema anamshukuru Mungu kwa sababu hana mume wala
mtoto kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa mwanzo angejenga picha mbaya sana
kwa mwanaye.
“Wakati nilipokuwa na matatizo nilijifunza mengi kwamba hakuna rafiki
wa kweli kwa sababu walinipenda nikiwa mzima lakini nilipokuwa naumwa
hakuna hata mmoja aliyenipigia simu kunijulia hali zaidi ya mashabiki
zangu tu kwa hiyo nimebadilisha mfumo wa maisha yangu,” alisema Ray C.
Miezi kadhaa iliyopita, mwanamuziki huyo alitangaza kuachana na
madawa ya kulevya ambayo alikiri kuwa yalimharibia mwenendo mzima wa
maisha yake.
No comments:
Post a Comment