MWIGIZAJI wa filamu na mwanamuziki wa kizazi kipya Snura Mushi mama
wa Majanga, amekanusha uvumi ambao umeenea kuwa ana mahusiano ya
kimapenzi na na mchezaji wa mabingwa wa ligi kuu Yanga sc Mrisho Ngasa,
Snura amesema kuwa alikuwa kimya bila kuongelea suala hilo lakini ameona
kuna baadhi ya watu wanataka kuhalalisha jambo hilo hivyo lazima
alikanusha kwa nguvu zote.
“Wapo wengi ambao najua watu watasema kuwa wacheza mpira ni mabwana
zangu lakini hakuna ninayetoka naye kimapenzi, mimi sitoki na Mrisho
Ngasa lakini nimefanya naye kazi ya filamu yangu ya Majanga sasa watu
wanatangaza kama Ngasa ni mtu wangu na natoka naye lakini Ngasa ni
msanii tu aliyeshiriki katika filamu yangu,”anasema Snura.
Snura anadai kuwa katika filamu yake ya Majanga Mrisho Ngasa kaigiza
kama mmewe au mchamba wake, hivyo iwe kwa bahati mbaya au kuna mtu
ambaye aliwaona katika baadhi ya picha na kutangaza kuwa ni wapenzi
amekosea msanii huyo anasisitiza kuwa Mrisho amemwigiza katika fani ya
uigizaji ni rafiki wa kikazi tu na si vinginevyo.
Msanii huyo ambaye anafanya vizuri katika filamu na muziki hivi sasa
nyota yake imeng’ara katika muziki na anatamba na kibao ‘Nimevurugwa’
huku kibao cha Majanga kukiendeleza kwa kukitungia filamu
iliyoshirikisha watu maarufu kama akina Mrisho Ngasa ambaye inasemekana
anatoka naye naye anasema ni filamu tu.
CHANZO NI FILAMU SWAHILI
No comments:
Post a Comment