EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, December 12, 2013

WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MTWARA WAKOSA MAHALI PA KUISHI


Meneja wa Vodacom kanda ya Kusini, Henry Tzamburakis akikabidhi msaada wa chakula kwa kituo cha wa watoto yatima cha EAGT Rahaleo Manispaa ya Mtwara Mikindani. Wanaopokea msaada huo kutoka (kushoto) ni watoto wanaoishi katika mazingira magumu Yasunta Rawland,  Boniface Seleman, Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto cha EAGT Mtwara, Caroline Mkwele, Askofu wa kanisa la EAGT Rahaleo Mtwara pia (mwasisi wa kituo) George Mrope. Vodacom kanda ya kusini inatarajia kutumia Tsh.Milioni 3 kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali katika jamii ya kanda ya kusini.

MTWARA, Mkurugenzi wa kituo cha Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT)  la Rahaleo Mtwara, Bi. Caroline Mkwele amesema kituo chake hakina majengo ya kuwalelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu takribani hamsini na tatu wanaolelewa na kituo hicho, hatua inayowalazimu watoto kuishi na walezi wao majumbani  nakupelekea  ugumu katika kuwalea katika maadili.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo wakati wafanyakazi wa  kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania walipo watembelea kituoni hapo na kukabidhi msaada wa chakula, fedha na vitu mbalimbali ambavyo vinatoka katika michango ya wafanyakazi kupitia mpango wa Pamoja na Vodacom unaolenga kutatua changamoto za ugumu wa maisha zinazoikabili jamii.
“Changamoto tulizo nazo ni nyingi lakini zaidi ni hili la kukosa kituo rasmi kwa maana ya majengo ya kuwahifadhi watoto hawa kwa pamoja, kwa sababu usipowaweka hawa watoto pamoja uwezekano wa kuwa na tabia tofauti ni mkubwa. Hivyo kutokana na ukosefu wa kituo inatulazimu kukutana na watoto hawa kila siku ya Jumamosi. Nawashukuru Vodacom kupitia Taasisi yao ya Vodacom Foundation kwa msaada huu, pia natoa wito kwa wafadhili wengine watusaidie watoto hawa, wasilifumbie macho tatizo hili.” Alisema Bi. Mkwele.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Meneja wa Vodacom Tanzania kanda ya kusini Henry Tzamburakis  amesema watoto yatima wanahitaji kupata elimu na mahitaji muhimu kama walivyo watu wengine hivyo  kampuni  yake  itaendelea kutoa msaada ili kuwapunguzia watoto hao ugumu wa maisha.

“Watoto hawa naweza kusema kwamba ni watoto wetu, wadogo zetu na ndugu zetu hivyo yatupasa kuwajali kwa kusikiliza mahitaji yao. Mimi binafsi ningependa kutoa wito tusingojee mpaka kampuni ijikusanye ndio tuje kutoa msaada, mtu yeyote anaweza kufanya hivi kwani haihitaji mpaka uwe tajiri sana, ukiwa na chakula, nguo, chochote kile ambacho unaona kitawafaa watoto hawa usisite kuwaletea.” Alisema Tzamburakis

Kwa upande wao watoto wanaolelewa na kituo hicho walibainisha kwamba si kupenda kwao kuwa yatima hali hiyo inaweza kumkuta yeyote yule ndani ya jamii, wanawasihi watu wenye uwezo wa aina yeyote kuwasaidia.

“Tunashukuru kwa msaada huu, kwa kweli utatusaidia siku zote za maisha yetu, nawaomba msife moyo kutusaidia kwani bado tunahitaji sana na pia tunathamini kwa kile mnachokifanya.” Alisema Boniface Seleman mmoja wa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha EAGT Rahaleo Mtwara

Naye mtoto wa kituoni hapo, Sofia Said alisisitiza kuwa “tunashukuru kwa msaada huu, nawasihi na wengine kuiga mfano waliouonesha kampuni ya Vodacom, zaidi ya hayo ningependa kusema asanteni sana.”

“Napenda kuwaambia wanajamii wenzetu kama unamuona mtoto yatima na wewe una uwezo hata kidogo, sio lazima iwe pesa hata chakula unamsaidia tu.” Alimalizia Yasunta Rawland ambaye pia ni mtoto yatima wa kituoni hapo

Kwa zaidi ya miaka kumi kampuni ya simu za mkononi Vodacom  imekuwa mstari wa mbele kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji maalumu ambapo katika kipindi hiki watoto zaidi ya 53 wanaolelewa na kituo EAGT Mtwara wamenufaika na msaada huo.

Ongezeko la watoto yatima limekuwa ni janga la kitaifa kwa muda mrefu nchini Tanzania huku serikali, taasisi, mashirika, makampuni binafsi na jamii kwa ujumla zikifanya jitihada mbalimbali za kupambana na kuondokana na changamoto hiyo inayotukabili.

Taasisi ya Vodacom Foundation imekuwa mstari wa mbele kushirkiana na serikali, mashirika, taasisi na wadau mbali mbali wa sekta za maendeleo nchini katika kuisaidia jamii ambayo kwa kiasi kikubwa ni wateja wake. Taasisi hiyo imejidhatiti kufanya kazi na kutoa ushirikiano wa aina yeyote kuhakikisha gurudumu la maendeleo la watanzania linasonga mbele kwa kasi inayotakiwa.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate