EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, December 14, 2013

UGOMVI WA KIMAPENZI WAPELEKEA MUME KUUA MTOTO WA KAMBO IRINGA

Mwenyekiti wa mtaa wa pangani kata ya Makorongoni mjini Iringa Salum Kibaya  akiutazama mwili wa mtoto Raymond Ben Mangungu (2)  aliyeuwawa kwa kukabwa  shingo  na baba wa kambo wakati wa ugomvi wa kimapenzi kati ya mwanaume  huyo na mama wa mtoto  huyo  usiku wa leo
Askari  polisi akitazama mwili wa mtoto  huyo
hali  ilivyokutwa ndani ya chumba  hicho  baada ya  tukio
Wananchi  wa Makorongini  wakimtazama  mwanamke huyo wakati akihojiwa na kaka wa mtuhumiwa wa mauwaji  hayo
Mama  wa mtoto Raymond katikati  akimsimulia shemeji  yake jinsi ambavyo mpenzi  wake  alivyoua mtoto ,kushoto ni mama mzazi wa mwanamke  huyo
Huyu  ndie mzazi wa mtoto aliyeuwawa  Bi Kudra Kahemela (23)
Mama  wa mtoto aliyeuwawa Kudra kahemela kushoto akiwa na mama  yake  mzazi katikati na dadake  kulia
Mmoja kati ya askari wa kike  kulia akimsaidia kumfunga kanga mama wa mtoto Raymond
Wanawake wa mtaa wa Pangani Iringa  wakiuhifadhi mwili wa mtoto Raymond leo
Polisi Iringa  wakiutoka  mwili wa mtoto Raymond leo
umati  wa wananchi  waliofika kushuhudia tukio  hilo leo
KATIKA  hali  isiyo ya kawaida mwanaume  mmoja mkazi  wa mtaa wa Pangani kata ya Makorongoni  katika Manispaa ya  Iringa Hamis Said maarufu kwa jina la Mwarabu amemuua  kinyama mtoto Raymond Ben Mangungu (2) kutoka  na ugomvi wa kimapenzi  kati  yake na mama  wa mtoto  huyo ambae kwake ni mpenzi wake .

Imedaiwa  kuwa  mtuhumiwa  huyo  wa mauwaji ya  mtoto  huyo  alikuwa amelewa  pombe  kupita  kiasi na si mara ya kwanza  kulewa kiasi  hicho na  kutishia kufanya mauwaji dhidi ya mtoto  huyo wa kambo kwa kile alichokuwa akidai  kuwa ni fedhea kwake  kuishi  na mwanamke ambae ana  watoto  wawili ambao si damu yake.

Wakizungumzia  juu ya  tukio hilo mashuhuda wa  tukio  hilo kwa sharti la  kutotaja majina yao  walisema  kuwa imekuwa ni kawaida  kwa Mwarabu kumpiga mwanamke  huyo na  familia yake kwa madai kuwa hataki kuwaona  watoto hao  wakiendelea  kuishi katika  nyumba hiyo ambayo ameipanga  yeye .

" Huyu  bwana Mwarabu alikuwa akifanya kazi ya kuuza korosho  mitaani na akirudi  usiku amekuwa  mkali kwa mwanamke  huyo ambae  alikuwa akidai kuwa bado amekuwa na mahusiano na baba  wa  watoto  hao  wawili .....hata  hivyo sisi kama majirani  tumekuwa  tukishindwa  kuwaamua kutokana na mwanaume  kuwa na tabia ya kulewa  pombe  kupita  kiasi na hata  tukio  hili tulijua ni kawaida  yao "

Mtoto  Tinito Mangungu (6) ambae  ni kaka  na  marehemu alisema  kuwa  baba yao  huyo mdogo alifika usiku na  kuwataka  wote  kuamka kitandani na  kuwa hakuna mtu atakayelala katika  chumba  hicho kama si  damu  yake.

"Baba mdogo  (Mwarabu) alirudi  usiku akiwa amelewa na kusema hakuna mtu  kulala kitandani na kuanza  kumpiga mama kwa meza na viti  huku sisi  tukilia kumtaka asimpige  mama yetu....baada ya hapo alimchukua mdogo  wangu na kuanza kumkaba  shingo na kumwacha  kitandani akiwa amelama bila kuamka  hadi  sasa mama anasema amekufa"

Akielezea  juu ya mkasa  huo  uliosababisha mauwaji  ya mtoto Raymond mama mzazi  wa mtoto  huyo Bi Kudra Kahemela (23) alisema  kuwa kwa upande  wake baada ya  kutishiwa kuuwawa kwa  kipigo alifanikiwa  kukimbia katika  chumba  hicho  na kwenda  kujificha  nje na baada ya muda mwanaume  huyo alianza  kutapika na pale  alipoingia kutana kumsaidia ndipo alipopigwa na kuamua kukimbia kwenda kulala nje ya nyumba  hiyo kwa  kujiegesha katika nguzo ya umeme  iliyopo nyumba ya pili karibu na nyumba ya  shekhe wa  mkoa Juma Alli Tagalile 

Alisema  kuwa asubuhi  aliingia katika  chumba  hicho baada ya mwanaume  huyo  kutoka kwenda katika kilabu  cha pombe za kienyeji  cha Tulivu  kuendelea  kunywa  pombe na  kumkuta mtoto  huyo akiwa amelala bila  kutikisika .

" Mimi  nilijua kama mtoto  amelala tu ama amezimia ila baada ya  kuwaita watu  wazima akiwemo mama yangu mzazi ndipo  nilipobaini  kuwa mtoto  wangu Ray amefariki  dunia na  ndipo  nilipomfuata na kumweleza juu ya tukio  hilo  ila bado  aliendelea  kunywa  pombe na kudai kuwa mtoto  huyo amezimia kwa  kelele za usiku ."

Alisema baada ya hapo mwanaume  huyo alikimbia hadi Ilala kwa wakwe  zake na kuomba msamaha na kusuluhishwa  ugomvi  wao  ila  wakati mtengo wa kukamatwa  ukiwekwa  ndipo alipokimbia kusiko  julikana.

Mwandishi  wa habari hizi  alishuhudia mtoto  huyo akiwa amekufa  katika  kitanda cha  wazazi  wake huku chini ya  chumba hicho  thamani mbali mbali pamoja na vyombo  vikiwa  vimevunjika kutokana na ugomvi  huo .

Mwenyekiti  wa serikali ya  mtaa  huo wa Pangani kata ya Makorongini Bw  Salum Kibaya  amethibitisha  juu ya  kifo  cha mtoto  huyo na kuwa baada ya  tukio  hilo ambalo  lilitokea  usiku wa kuamkia  leo jumamosi Desemba 14 mwaka  huu alilazimika kwenda  kituo cha polisi  cha stendi  kuu ya mabasi yaendeyo mikoani na kuwajulisha  juu ya tukio  hilo na kufika  eneo  la tukio .

Bw  Kibaya  alithibitisha  pia  kuwa ugomvi kati ya wapenzi hao  si wa kwanza  kutokea  japo kwa maelezo ya  mwanamke  huyo alikuwa mbioni  kuolewa na mwanaume  huyo na hivyo kuwa na wanaume  wawili akiwemo mzazi mwenzake ambae kwa  sasa anaishi  eneo la Don Bosco mjini hapa.

Mwili  wa mtoto   huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa  wa Iringa  huku jeshi la polisi likiwahoji  mama  wa mtoto  huyo ,kama  wa mtuhumiwa wa mauwaji  hayo ambae ni mkazi wa Mlandizi Kibaha Jijini Dar es Salaam  na mama mzazi  wa mtoto aliyepoteza maisha.
CHANZO NI MZEE WA MATUKIO - FRANCIS GODWIN

1 comment:

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate