Ligi Kuu ya England mwaka huu ni shughuli pevu.
Jumamosi, Chelsea alikuwa kileleni, Jumapili, Manchester City na sasa ni Arsenal. Kiasi cha pointi mbili tu kinazitenganisha timu tatu za juu. Kikosi cha Arsene Wenger kimerejea kileleni kufuatia ushindi wa mabao 2-1 ugenini usiku wa kuamkia leo dhidi ya Aston Villa. Jack Wilshere alifunga dakika ya 34 na Olivier Giroud akafunga la pili dakika ya 35 Arsenal ikaongoza 2-0 kabla ya Cristian Benteke kuifungia Villa la kufutia machozi dakika ya 76.Arsenal inarejea kileleni kwa pointi zake 48, ikiishusha Manchester City yenye pointi 47 katika nafasi ya pili, mbele ya Chelsea yenye pointi 46.

No comments:
Post a Comment