KOCHA Franciscus ‘Hans’ van der Pluijm ametua jijini Dar es Salaam, akiwa na asilimia 90 za kuwa kocha mpya wa mabingwa wa Tanzania, Yanga.
Van der Pluijm, raia wa Uholanzi, ndiye chaguo la kwanza la Yanga katika makocha watatu walioingia fainali, wengine ni raia wa Sweden na Ubelgiji, kocha huyo alitua nchini jana saa tatu asubuhi na moja kwa moja akapelekwa hotelini.

Baada ya hapo, mazungumzo yalifanyika katika hoteli moja saa 5
asubuhi akiwa na watu wa kamati inayohusiana na masuala ya usajili.
Mazungumzo kati ya van der Pluijm na viongozi hao wa Yanga
yalikatishwa ili kumpa nafasi ya kupumzika na baadaye saa 10 jioni
wakakutana tena.
Tayari mazungumzo yamezaa matunda, ameshakubaliana kila kitu na Yanga, leo Jumatatu asubuhi anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili.
Tayari mazungumzo yamezaa matunda, ameshakubaliana kila kitu na Yanga, leo Jumatatu asubuhi anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili.
Baada ya kusaini mkataba, kocha huyo ataelekea Zanzibar kuiangalia
Simba iliyo chini ya Zdravko Logarusic ikicheza fainali ya Kombe la
Mapinduzi dhidi ya KCC ya Uganda.
Pluijm aliwahi kusababisha Logarusic akatimuliwa wakati Mcroatia huyo alipokuwa akifundisha timu moja Ghana na Pluijm akamfunga 4-1 alipokuwa Berekum Chelsea.
Pluijm aliwahi kusababisha Logarusic akatimuliwa wakati Mcroatia huyo alipokuwa akifundisha timu moja Ghana na Pluijm akamfunga 4-1 alipokuwa Berekum Chelsea.
Ijumaa
iliyopita, Championi kilikuwa chombo cha habari cha kwanza kuandika
kuhusu kocha huyo aliyetengeneza jina nchini Ghana kuanza mazungumzo na
Yanga.
“Kama tungeshindwa kuelewana na van der Pluijm, basi mara moja
tungemfuata kocha mwingine ambaye ni Lars Olof Mattsson, raia wa
Sweden,” kilieleza chanzo cha uhakika.
“Unajua kuona CV ya mtu na kukutana naye uso kwa uso ni vitu viwili tofauti. Ile kuzungumza naye unaweza kujifunza kitu, ndicho tunachofanya.”
“Unajua kuona CV ya mtu na kukutana naye uso kwa uso ni vitu viwili tofauti. Ile kuzungumza naye unaweza kujifunza kitu, ndicho tunachofanya.”
Van der Pluijm alipata
mafanikio makubwa akiwa na Berekum Chelsea ya Ghana katika msimu wa
2012-13 katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha aliyekuwa akipewa nafasi ya tatu kuinoa Yanga ni Luc Eymael raia wa Ubelgiji na huyo ni kama Jangwani wangeshindwana na “The Choosen One”.
Kocha aliyekuwa akipewa nafasi ya tatu kuinoa Yanga ni Luc Eymael raia wa Ubelgiji na huyo ni kama Jangwani wangeshindwana na “The Choosen One”.
CHANZO NI CHAMPIONI JUMATATU
No comments:
Post a Comment