KOCHA mpya wa Yanga, Hans van Der Pluijm, ameweka rekodi mpya akiwa na klabu yake hiyo nchini Uturuki.
Kocha huyo Mholanzi ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza wa klabu kutoka nje ya Tanzania kuvaa sare ya timu ya taifa, Taifa Stars.
Kwa kipindi chote ambacho Yanga wamekuwa nchini Uturuki, van Der Pluijm amekuwa akivaa koti la Taifa Stars ambalo huvaliwa na wachezaji na makocha wa kikosi hicho kinapokuwa kwenye mashindano.
Bila ya kujua amelitoa wapi, picha zinazotumwa kutoka Antalya, Uturuki zinaonyesha van Der Pluijm akiwa amevaa koti hilo la rangi ya bluu na mistari midogo ya njano.
Ingawa Yanga inatumia rangi za njano na kijani, lakini van Der Pluijm amekuwa akionekana na koti hilo anapokuwa kazini na wachezaji wa Yanga.
Hakuna kocha yeyote wa Yanga, Simba, Azam FC au Coastal Union ambaye amewahi kuonekana kutumia kifaa cha Taifa Stars.
Kwa mara ya kwanza, kocha huyo ataonekana akiwa na kikosi cha Yanga kwenye mechi ya ufunguzi wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara itakapokutana na Ashanti United, Jumamosi.
No comments:
Post a Comment