Kumshangaza huko kumekuja baada ya Lulu kufika nyumbani kwa mama Kanumba, Kimara Temboni jijini Dar akiwa na bonge la keki, jambo ambalo mama huyo hakulitarajia.
“Yaani mama Kanumba alikuwa hajui kuwa Lulu anajua siku yake ya kuzaliwa, Lulu akatumia nafasi hiyo kumfanyia ‘sapraizi’,” alisema rafiki wa karibu wa Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Waandishi wetu waliokuwa eneo la tukio walimshuhudia mama Kanumba akiwa amepigwa na butwaa huku akilengwalengwa na machozi ya furaha. Mahojiano yalifanyika kama ifuatavyo;
Ijumaa: Hongera mama, sasa unatimiza miaka mingapi?
Mama Kanumba: Nimetimiza miaka 58.
Ijumaa: Umejisikiaje kwa zawadi ya keki uliyoletewa na Lulu?
Mama Kanumba: Nimejisikia furaha sana kwa kweli, Lulu ni mwanangu, nimefarijika, kwa sababu watoto wangu hawapo, leo ningekuwa peke yangu lakini kama unavyoona, mama na mwanaye wamekuja toka asubuhi tunasherehekea nao kwa kula na kunywa na Lulu amegharamia kila kitu.
Baada ya swali hilo Ijumaa lilihamia kwa Lulu.
Ijumaa: Ulijuaje leo ni siku ya kuzaliwa ya mama Kanumba?
Lulu: Nilijua katika maongezi siku sita zilizopita, kwani ilikuwa ni tarehe moja ya mwezi huu ambapo amezaliwa mama yangu mzazi na dada yangu.
Ijumaa: Kwa nini uliamua kumfanyia Sapraizi ya keki mama Kanumba?
Lulu: Niliamua kumfurahisha kwa sababu ni siku yake ya kuzaliwa na sikufanya kwa sababu mwanaye hayupo, hata angekuwepo ningemfanyia tu.
Ijumaa: Asanteni, mama na Lulu tunawatakia maisha mema.
CREDIT:GPL
No comments:
Post a Comment