BAADA ya kuzagaa kwa fununu za chini ya kapeti kuwa
mastaa wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi na Chuchu Hans kutarajia
kufunga ndoa, wenzao wa Bongo Movie wameonesha hadharani kuwa wanaiunga
mkono ndoa hiyo na kutoa baraka zao.
Tukio hilo lilijidhihirisha wazi hivi karibuni katika Viwanja vya
Leaders Club, Kinondoni jijini Dar katika uchaguzi wa viongozi wa Klabu
ya Bongo Movie ambapo Ray ambaye alikuwa mwenyekiti mstaafu wa klabu
hiyo, aliambatana na ‘bebi’ wake huyo (Chuchu) na kupozi katika staili
ya ‘mista na misezi’.
Bila kupepesa macho, kwa nyakati tofauti mastaa hao waliokuwa
wakifuatilia uchaguzi huo, wa kiume walimuita Chuchu shemeji huku wa
kike wakimuita Chuchu wifi ambapo bibie aliitikia bila hiyana.
“Tunajua kuwa Ray na Chuchu ni wapenzi na tuko tayari kushuhudia ndoa
yao na tutatoa mchango wowote utakaohitajika kwa ajili ya kufanikisha
harusi yao kwani wanaonekana kupendana, tangu nianze kuona uhusiano wa
wasanii hakuna hata mmoja aliyewahi kuwa na mapenzi ya dhati kama
wanayoonesha Ray na Chuchu,” alisema mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi
ya jina.
Staa mwingine mwenye ‘taito’ kubwa ndani ya Bongo Movies, kwa sharti
la kutotaja jina lake alisikika akisema: “Ray na Chuchu wanaonyesha
penzi lisilo na unafiki hata chembe, kama ilivyozoeleka kwa wasanii
wengine na ndiyo maana leo utaona wanaenda sehemu zote wakiwa pamoja na
wala hawajifichi kwa lolote lile.”
Kuonesha kuwa wanapendana, Chuchu alionekana kumrekebisha nguo vizuri
Ray kila alipogundua imekaa vibaya huku wakichagiza ‘malovee’ yao kwa
‘hagi’ na kukumbatiana kwa kishkaji.
No comments:
Post a Comment