EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, January 29, 2014

MKUNGA WA JADI ALIYEFANIKIWA KUMZALISHA MWANAMKE WATOTO WATATU AOMBA MSAADA WA VIFAA VYA KUZALISHIA

WADAU wa sekta ya Afya nchini wametakiwa kuwajali na kuwathamini wakunga wa Jadi kwa kuwa wamekuwa wakombozi kwa wazazi waishio mbali na vituo vya afya pindi wanapohitaji huduma ya kujifungua. Mwito huo ulitolewa na Mkunga wa Jadi, Dotea Mwanakulya (60) Mkazi wa kijiji cha Magamba Wilayani Chunya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea nyumbani kwake kujua changamoto anazokabiliana nazo. Mkunga huyo wa alisema anakabiliwa na changamoto za ukosefu wa vifaa vya kujifungulia kama kitanda,godoro,mipira ya kuvaa mikononi ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa ambapo wagonjwa wengine hufika hapo wakiwa hawana vifaa  hivyo. Hata hivyo mkunga huyo amewaomba wadau mbali mbali kumsaidia kupata daftari ya kutunza kumbukumbu za watoto wanaozaliwa nyumbani kwake kwa kile alichodai kuwa hana kumbukumbu sahihi za idadi hali ya watoto waliozaliwa kwake. Mkunga huyo alilazimika kutoa kauli hizo kufuatia kuwepo kwa Mwanamke mmoja kujifunga watoto mapacha mfululizo kwa Mkunga huyo na watoto wake wakiendelea kukua vizuri. Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Paskalia Adrofu (37)mkazi wa kijiji cha Magamba kata ya Magamba wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,alijifungua salama watoto watatu hivi karibuni kwa mkunga wa Jadi huyo. Paskalia amejifungua watoto wawili jinsi ya kiume na mmoja wa kike ambapo amesaidiwa  na mkunga wa jadi  Dotea Mwanakulya (60)anayeishi kijiji cha Magamba. Paskalia alisema kwamba mume wake aitwaye Richard Saba (55) ni mkulima hivyo imekuwa vigumu kwake kumudu gharama za matunzo kwa watoto hao ambapo ana jumla ya watoto wanane,wakiwemo mapacha ambao wamemaliza shule ya msingi na hawajachaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari. Mama huyo alianza kujifungua mtoto wa kwanza mwaka 1995,wa pili ambao ni mapacha mwaka 1998 wa tatu mwaka 2006,wa nne mwaka 2009 na wa tano ambao wamezaliwa watatu amejifungua mwanzoni mwa mwaka huu ambao wana afya njema. Hata hivyo Paskalia alisema uongozi wa kata akiwemo Diwani wa kata ya Magamba  Chakupewa Kapalala wamefika kumtembelea na kumjulia hali yake na kumhimiza kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili kufuatilia afya za watoto. Aidha mkazi mmoja wa kijiji hicho aitwaye Luhende Luhaga ametoa ng’ombe wawili wa maziwa ili mama huyo amudu kuwanyonyesha watoto hao bila shida kutokana na kulemewa na watoto hao. Watoto wawili wa mwanzo wamezaliwa na uzito wa kilo 2.8 na wa tatu amezaliwa na uzito wa kilo 2.0 ambapo Paskalia alisema kuwa watapofikia uzito wa kilo 3 ndipo watapatiwa chanjo katika zahanati ya Magamba. Baadhi ya changamoto anazokabiliwa nazo ni pamoja na nguo za watoto,chupa za kunyonyeshea,sabuni,mafuta na chupa za chai kwa ajili ya kuhifadhia maziwa ya watoto. Na Ezekiel Kamanga Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate