Marehemu
Mzee Arnold Wilfred Nkhoma Kambonapany (kulia) enzi za uhai wake akiwa
na mmoja wa watoto wake kwenye ibada maalum ya kutoa shukrani
alipotimiza miaka 100 iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Andrea
Magomeni jijini Dar hivi karibuni.
Familia
nzima ya Nkhoma Kambonapany wanasikitika kutangaza kifo cha baba na
babu yao mpendwa Mzee Arnold Wilfred Nkhoma Kambonapany, kilichotokea
kwenye hospitali ya Mount Ukombozi tarehe 17/01/2014.
Taarifa
za msiba ziwafikie Doctors Colin na Nicholas Darch wa Cape Town Afrika
Kusini , Bi Laura Amrei wa Hamburg Ujerumani , Bi Ajira Darch wa San
Fransisco , California , Marekani , Bwana Monday Wamunza akiwa Maryland ,
Marekani , ndugu na jamaa popote walipo.
Alijaliwa
kupata watoto 11, wajukuu 36 , na vitukuu 25. Msiba unafanyika kwa
mtoto wake Professor Alice Wamunza Nkhoma , Nyumba na. 07 , Mtaa wa
Koroshoni , Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Maziko yatafanyika tarehe leo 19/01/2014 kwenye makaburi ya Kinondoni.
Msafara
wa mazishi utaanzia saa tano za asubuhi chuo kikuu baada ya chakula na
kutoa heshima za mwisho. Baada ya hapo utaelekea Kanisa la Mtakatifu
Andrea Magomeni kwa ajili ya Misa.
Baada ya hapo utaelekea Kinondoni makaburini kwa kumpumzisha Mzee Kambonapany.
No comments:
Post a Comment