EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, February 5, 2014

BIFU LAO KWA DIAMOND... JOKATE AMWANGUKIA WEMA


WERAWERAA! Staa wa Bongo anayesumbua kwenye mitindo na sinema, Jokate Mwegelo amekubali kushindwa baada ya kumwangukia Wema Sepetu waliyekuwa kwenye bifu la kimyakimya wakigombea penzi la Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Jokate akiwa sambamba na Wema.
Tukio hilo la kufungulia mwaka lilijiri wikiendi iliyopita jijini Arusha, katika kiwanja cha kulia bata, Triple A Club ambapo Wema alikuwa akimtambulisha mwanamuziki Miraji Hussein ‘Mirror’ kutoka Lebo ya Endless Fame Production.
Wema aikumbatiana na Jokate.

BONGE LA SAPRAIZI
Mwandishi wetu ambaye alikuwa katika msafara wa Wema na mashosti zake, Kajala Masanja na Aunt Ezekiel waliokuwa wakimpa kampani, hakumuona Jokate, hivyo alifika pale kwa kushtukiza.
Jokate akionekana mwenye furaha, alipanda jukwaani na kuomba kuzungumza machache ambapo alimkumbatia Wema kwa furaha huku akionekana hana kinyongo.
Jokate baada ya kupanda stejini na kumfuata Wema.
AKIRI WEMA NDIYE MKE MKUBWA
“Wema ni rafiki yangu na ninampenda kwa dhati... yaliyopita yamepita. Nipo hapa kwa ajili ya kumpa sapoti kutokana na upendo nilionao juu yake. Nakiri  yeye ni mke mkubwa. Nimeamua kumshtukiza ili aone thamani yake kwangu.”
Maneno hayo ya Jokate yalisababisha ukumbi mzima ulipuke kwa kelele za shangwe.
Jokate akianza kummwagia manoti Wema.
AMWAGA MINOTI
Kama vile haitoshi, huku shangwe zikiendelea, bidada huyo alitoa burungutu la fedha na kuanza kumtuza Wema.
Mamaa Kidoti akizidi kutoa 'misimbazi' kwa Wema.
Pia aliwatuza Kajala na Aunt ambao wote kwa pamoja walikuwa wamevaa sare kama kinogesho cha shughuli hiyo.
Wapambe wakikusanya minoti iliyomwagwa na Jokate.
JOKATE ABANWA
Risasi Mchanganyiko halikuishia kufotoa picha na kuweka gazetini pekee, lilimfuata Jokate na kumwuliza sababu ya kufanya tukio hilo ambapo alijibu kifupi: “Ni upendo tu dadangu.”
Minoti iliyotapakaa stejini ikizidi kukusanywa.
Alipobanwa zaidi alisema: “Mimi niliona nikifika kumpa kampani mwenzangu itapendeza sana na sikutaka ajue mapema ili ujio wangu umshangaze. Nimefurahi imekuwa hivyo.”
Jokate akiendelea kuonyesha jeuri ya fedha kwa kumtunza shosti wake Wema.
WEMA SASA!
“Yaani nimefurahi sana kuona Jokate anajua kuwa mimi ni mke mkubwa na ndiyo kila kitu,  nimefurahi kuacha kazi zote kuja kuungana nami, kitu ambacho nimekiona tofauti kwani hatukuwahi kukaa hivyo na Jokate tangu tulivyoingia kwenye mgogoro (wa kumgombea Diamond),” alisema Wema.
Ilikuwa 'misimbazi' tupu!
WEMA / JOKATE
Upinzani wa Wema na Jokate ulianza kitambo kwani mwaka 2006, Wema ndiye aliyeibuka Miss Tanzania akifuatiwa na Jokate aliyeshika namba mbili huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Lisa Jensen.
Jokate akishangiliwa na mashabiki.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate