KANUNI ZA KUEPUKA KUZINI NJE YA NDOA AU MPENZI WAKO..!
Leo tuende moja kwa moja kuangalia baadhi ya mambo ambayo yaweza kukusaidia kuepuka kuzini nje ya ndoa yako au kutoweza kumsaliti mpenzi wako.
1. KUJIEPUSHA KUWA KARIBU NA JINSI ZINGINE UKIWA UMELEWA
Hapa nitoe ufafanuzi wa jambo moja la jinsi ambapo nazungumzia masuala ya maumbile ambapo wengi wetu tunachanganya neno jinsi na Jinsia.
Kuepuka kuwa karibu na jinsi tofauti nawe ni suala gumu sana lakini ni vema unapokuwa unakula maji(kilevi) ni vema ukawa makini kuwa mbali na mtu wa jinsi nyingine ili kuepukam kupata vishawishi na kumsaliti mwenzi wako.
2.EPUKA MAZUNGUMZO YA KIMAHABA
Ni njia rahisi sana inayoshawishi watu wengi kujiingiza kwenye usaliti ama mapenzi mapya ambapo endapo hautakuwa makini na kujiingiza katika mazungumzo ya kimahaba na mtu wa jinsi nyingine unaweza kujikuta unajiingiza katika usaliti wa kimapenzi lakini njia hii licha ya kuwa ni njia moja wapo ya kuepuka usaliti ni njia nzuri ya kuanzisha mapenzi mahusiano mapya ambapo wengi hushawishika na kujikuta kutamani kupata vitu vipya katika mahaba ambavyo mtu aliyenaye kwa muda huo amevigusa katika mazungumzo yao.
3.KUWA MKWELI
Ukweli ni jambo muhimu katika kudumisha mahusiano na kuepuka usaliti kwasababu mwenzi wako anaweza kuhisi kitu kuwa umeanzisha mahusiano na mtu mwingine ambaye mara kadhaa mnafanya nae utani, hivyo ni vema ukawa mkweli kwa mwenzi wako kumweleza kuwa mtu huyo mnafanya masihara nae na wala hakuna jambo lolote linaloendelea kimahusiano tofauti na kutumia lugha kama ‘’Kwani unafikiri mimi nafanya nini nae’’ hilo jibu si sahihi katika kuboresha mahusiano yenu.
No comments:
Post a Comment