Kadi mpya ya malipo ya matibabu katika Hospitali ya KCMC inavyoonekana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB akizungumza wakati wa uzinduzi wa KCMC Tembo Card itakayotumika kwa ajili ya malipo ya matibabu katika hospitali ya KCMC.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dk. Martin Shao akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi ya malipo ya KCMC Tembo Card kwa ajili ya malipo ya matibabu katika hospitali ya KCMC badala ya fedha taslimu.
Baadhi
ya maofisa wa Benki ya CRDB, wakiwa katika uzinduzi huo. Kushoto ni
Mkurgenzi wa benki ya CRDB tawi la Arusha, Chiku Issa na wa pili kulia
ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo Mikubwa, Philip Alfred.
Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya KCMC.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akimkabidhi KCMC
Tembo Card, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dk. Martin Shao, itakayowawezesha wagonjwa
wanaofika katika Hospitali ya KCMC kulipia huduma za matibabu kwa njia
ya kadi badala ya fedha taslimu. Uzinduzi huo ulifanyika mjini Moshi,
mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
hiyo, Prof. Raimos Olomi.
Mkuu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya
Kaskazini, Askofu Dk. Martin Shao akikata utepe wakati wa uzinduzi wa
malipo ya matibabu kwa kutumia kadi ijulikanayo KCMC Tembo Card katika
hospitali ya KCMC mjini Moshi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati), akiwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dk. Martin Shao.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini , Askofu Dk. Martin Shao akilipia
huduma za matibabu katika Hospitali ya KCMC kwa kutumia kadi maalum ya
KCMC Tembo Card badala ya fedha taslimu, wakati wa uzinduzi wa huduma
hiyo uliofanyika mjini Moshi.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dk. Martin Shao akionesha kadi ya malipo ya matibabu katika hospitali ya KCMC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akifanya malipo ya matibabu kwa njia ya kadi badala ya fedha taslimu.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC, Prof. Raimos Olomi akilipia
matibabu katika hospitali hiyo kwa kutumia kadi maalum ya KCMC Tembo
Card.
Dk. Kimei akipanda mti wa kumbukumbu.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Baadhi ya watu wakishuhudia uzinduzi huo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya uzinduzi wa KCMC Tembo Card mjini Moshi.
Dk.Charles
Kimei akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya
wateja wakubwa wa benki iliyofanyika katika ukumbi wa Kuringe mjini
Moshi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu, IGP Said Mwema akipata chakula wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC, Prof. Raimos Olomi (kulia) na Mkurugezni wa CRDB, Dk. Charles Kimei wakipata chakula.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi mstaafu (IGP), Said Mwema (wa nne kushoto), akicheza
ngoma za asili za kabila la wachaga wakati wa hafla ya chakula cha jioni
kilichoandaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wateja wa benki hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia), akiwa na Mkurugenzi wa tawi la CRDB Arusha, Chiku Issa wakati wa hafla hiyo.
MOSHI, Tanzania
BENKI
ya CRBD imezindua mpango mpya wa huduma za kulipa kabla kwa kutumia
kadi za benki hiyo katika hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mjini
Moshi. kwa lengo la kurahisisha malipo yanayotolewa kwa wagonjwa na
kuongeza mapato ya hospitali. Kutokana na uzinduzi huo wa kadi hiyo mpya
sasa huduma zitaweza kupatika kwa urahisi kwa wagonjwa ambao ni wateja
wa benki hiyo watakapokuwa wanapata huduma katika hospitali hiyo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dk Charles Kimei
alisema Benki kuongeza na kuboresha huduma zake nchini kwa kasi ili
iweze kuwafikishia wananchi wa kila aina huduma hizo ili kurahisisha
maisha yao. TemboCard KCMC Card’ sasa itakuwa
niKadi ambayo itakuwa ni suluhisho la ukusanyaji fedha za malipo ya
huduma katika hospitali hii ya rufaa ya KCMC.
Aliongeza
kuwa uzinduzi huu wa TemboCArdKCMC utasaidia kurahisisha malipo na
kuiwezesha hospitali hiyo kusimamia vema huduma zake kwa masualla
yanayohusu kipesa kwani kupokea pesa au kufanya shughuli za malipo
katika eneo lenye mchanganyiko wa shughuli kama katika Hospitali hii
lina changamoto nyingi zikiwemo zile za kupata noti bandia pamojan a
gharama kubwa za kusimamia.
Kwa mujibu wa Dk Kimei, matumizi ya TemboCard kadi za kulipia kabla kwa kiasi kikubwa kupunguza idadi ya shughuli za fedha katika hospitali , kwa kuzingatia kwamba zaidi ya asilimia 50 ya shughuli za kila siku katika hospitali ni kimsingi ni za kifedha hivyo kwa kutumia Tembocard KCMC kadi, wagonjwa watafanya shughuli za malipo katika vituo vilivyoko ndani ya hospitali na kupata risiti haraka na rahisi ," Dk Kimei alisema.
Mkurugenzi Mtendaji huyo pia alisisitiza kuwa Benki ya CRDB ina lengo kuimarisha usalama wa fedha kwa wateja na ina mifumo jumuishi kupatanisha shughuli yoyote katika muda halisi. Vile vile, benki imetumia teknolojia rahisi katika benki kadi hivyo kufanya Benki ya CRDB Tembo Cards salama zaidi .
Kimei alimwambia mgeni rasmi Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Dayosisi ya Kaskazini Dr. William Shao Askofu kuwa benki hiyo sasa imepata mafanikio
na ubora wa kimataifa wa kadi za ‘TemboCard” hivyo kupelekea mashirika
makubwa na ya kimataifa ya biashara ya kadi za malipo duniani yaani
Visa International, MasterCard na China Union Pay kujenga imani na
kuvutiwa kujiunga CRDB.
Aliweka
bayana kuwa Muungano huo ndio uliopelekea kuzalishwa kwa kadi za
TemboCardVisa, TemboCardMasterCard na sasa TemboCard-China Union Pay.
CRDB hadi sasa ni benki pekee katika Afrika nzima kuweza kuunganisha
jina la kadi yetu yaani ‘’Co-branding” na kadi hizi za malipo za
kimataifa. Hiki ni kithibitisho tosha cha ubora wa kimataifa wa kadi
zetu.
Dk Kimei alimhakikishiaAskofu Shao kuwa Kwa
wale ambao hawana akaunti za mabenki wala kadi za kimataifa, wao
watahitajika kuchukua kadi hizi za TemboCard-KCMC ambazo zitapatikana
Kwenye tawi lililopo hospitalini KCMC au kwenye tawi lolote la Benki
ya CRDB Moshi mjini, Marangu na Boma au vile vile kupitia kwa mawakala
wetu wa FahariHuduma waliopo kila kona.
Dk
Kimei alieleza upatikanaji wa kadi hizo kwa watu wanaopata huduma KCMC
kuwa zitatolewa bure kabisa ila wateja watakapozichukua, watalazimika
kuziwekea pesa tayari kwa malipo. Kadi hizi zinaweza kujazwa pesa kwa
kupitia njia mbalimbali kama Kuingiza pesa kwenye kadi hiyo kupitia
matawi yetu, Kuhamisha moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zao kwa
kutumia SimBanking au Kwa kutumia njia za mitandao ya simu yaani M-pesa,
TigoPesa na Airtell money.
Kimei
alizisifu kadi hizo kuwa za TemboCard KCMC kuwa zina ulinzi wa hali
juu hivyo mteja awapo na kadi hiyo asiwe wasiwasi kabisa na usalama wa
fedha zake. Kwani hata ikitokea kwa bahati mbaya mteja akaipoteza kadi
yake, hakuna mtu mwingine anayeweza kuitumia kwakuwa inatumia teknolojia
ya CHIP na PIN ambayo hairuhusu mtu asiyemuhusika kuweza kuitumia.
No comments:
Post a Comment