Mkurugenzi Msaidizi wa
Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas Mwaisobwa
akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam
Mkurugenzi
Msaidizi wa
Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas
Mwaisobwa
akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhusiana na
masuala ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini. Pamoja
nae
ni Ofisa Mwandamizi Habari, elimu na mawasiliano, Veneranda Malima.
*********
1.0 UTANGULIZI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu ilianzishwa kwa sheria Na. 9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi
majukumu yake Julai 2005. Bodi ina majukumu makuu mawili; kwanza ni kutoa
mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu kwa
ajili ya masomo ya Shahada au Stashahada ya juu.
2.0
UTOAJI
WA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Tangu kuanzishwa kwake, Bodi
imefanikiwa kutoa mikopo kwa idadi kubwa ya Wanafunzi ikilinganishwa na hali
ilivyokuwa kabla Bodi haijaanzishwa. Mwaka 2005/2006 Bodi ilipoanza kazi ilitoa
mikopo kwa Wanafunzi 42,729 wa elimu
ya juu kwa kutumia bajeti shilingi Bilioni
56.1.
Idadi ya Wanafunzi wa elimu ya juu
wanaopewa mikopo imeendelea kuongezeka kutoka
wanafunzi 42,729 mwaka 2005/2006
hadi Wanafunzi 97,348 mwaka 2012/2013.
Hii ni sawa na ongezeko la wastani wa 10.4%
kwa mwaka. Mikopo iliyotolewa
kwa Wanafunzi wahitaji iliongezeka kutoka TZS
56.1 Bilioni mwaka 2005/2006 hadi TZS
306 Bilioni mwaka wa fedha 2012/2013.
Kwa mwaka wa masomo 2013/2014,
jumla ya wanafunzi 95,178
wamenufaika na mikopo hadi kufikia tarehe 15 Machi, 2014 ambao mikopo ya kiasi
cha TZS 223,977,042,853.00 imekwishalipwa.
Mwaka
|
Idadi
ya Wanafunzi Waliokopeshwa
|
Ongezeko
(%)
|
Kiasi
kilichoko-peshwa
(Tshs
Bilioni)
|
Ongezeko
(%)
|
2004/05 (Na
Wizara)
|
16,345
|
-
|
9.9
|
-
|
2005/2006
|
42,729
|
161.4
|
56.1
|
467
|
2006/2007
|
47,554
|
11.3
|
76.1
|
35.7
|
2007/2008
|
55,687
|
17.1
|
110.8
|
45.6
|
2008/2009
|
58,798
|
5.6
|
139.0
|
25.5
|
2009/2010
|
72,035
|
18.4
|
237.8
|
28.7
|
2010/2011
|
92,791
|
28.8
|
230.0
|
24.5
|
2011/2012
|
94,533
|
2.0
|
311
|
35.0
|
2012/2013
|
97,348
|
2.9
|
335.2
|
7.2
|
No comments:
Post a Comment