EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, March 12, 2014

BONGO MUVI KUNA MASHOGA!

IMEBAINIKA kuwa ndani ya tasnia ya filamu Bongo kuna baadhi ya wasanii wanaofanya mapenzi ya jinsia moja yaani mashoga, Risasi Mchanganyiko limenyetishwa.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Hilo limeibuka ikiwa ni siku chache baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museven, kupitisha sheria nchini mwake ya kupiga marufuku mavazi yasiyo na staha, uvunjifu wa maadili na mapenzi ya jinsia moja.
Uganda ipo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiunganishwa na nchi za Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda yenyewe.
HABARI KAMILI
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vilivyomo ndani ya kundi hilo, baadhi ya wasanii wa kiume wanadaiwa kuwa ni mashoga, ingawa wanajifanya vidume vya mbegu.
“Wapo mashoga na mabwana zao tunawajua ila sema sasa kwa sababu huna ushahidi wa moja kwa moja na hujamfuma kwenye tukio, unashindwa kumtaja,” alisema msanii mmoja wa kike, Bongo.
“Yule…(analitaja jina la msanii mkubwa) bwana’ke alifariki na sasa ana mwingine lakini ndani ya Bongo Muvi anaonekana kiwembe kwa sababu ana msururu wa wanawake,” alisema.
AMSHAURI JK

“Ingekuwa vyema sana kama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akafanya kama alivyofanya mwenzake wa Uganda, Yoweri Museven katika kupiga vita ushoga,” alipendekeza msanii huyo.
Msanii mwingine wa kike ambaye amekuwa kwenye tasnia hiyo tangu enzi za makundi ya sanaa kutamba runingani (jina kapuni) naye alikiri kuwepo kwa ishu hiyo lakini akadai wanafanya kwa siri sana.
“Kuna wasanii wanaonekana watanashati mbele ya jamii lakini ni chakula ya watu kwa kuwa wanapenda sana vitu vya bure,” alisema msanii huyo na kuongeza:
“Wapo wengi tu ndiyo maana katika maisha yangu sijawahi kutoka na mwanaume wa Bongo Muvi, ni wachafu sana. Siku zote wasanii wa kike ndiyo tunaoambiwa kuwa ni malaya, eti tuna tamaa na habari nyingi zinatuchafua siye lakini ukweli ni kwamba hata wanaume wana tamaa ya maisha mazuri na mwishowe wanageuzwa wanawake.”
HUYU YUPO TOFAUTI NA WENZAKE
“Sikia nikuambie, ni kweli hili suala lipo lakini si kwa wote na kuna baadhi huwa wanasingiziwa tu. Unajua nini? Unaweza kukuta mtu ana tabia tu ya kujipenda, lakini wengine wanasingizia kuwa eti ni mashoga – siyo kweli.
“Mfano hata uje na greda hapa, akitokea mtu anazungumza upuuzi eti JB, Dk. Cheni, Ray, Hemed PHD, Mlela au Dude ni mashoga, nitabishana nao mpaka mwisho. Hao ni watu ambao wanajipenda tu, sasa ukiwahusisha na huo ujinga nitashangaa sana. Sisemi kuwa wanatajwa ila sasa akitokea mjinga akaja na hoja hiyo, nitabishana naye,” alisema msanii mmoja ndani ya Bongo Muvi.
Msanii Hisani Muya ‘Tino’ aliwahi kuigiza kama shoga na kusababisha minong’ono kwenye jamii, katika filamu aliyoipa jina la Shoga lakini ilizuiwa na serikali.
Mwingine ni Dk. Cheni ambaye amecheza kama shoga kwenye filamu yake ya Nimekubali Kuolewa, ingawa bado haijatoka mpaka sasa.
Msanii huyo akizungumzia hayo, alisema: “Kucheza filamu kama shoga hakuna maana kuwa kweli ni shoga, ni kuvaa uhusika tu. Watu wasiwahusishe wasanii walioigiza kama mashoga kwenye hii skendo,” aliweka nukta msanii huyo mwenye maneno mengi.
WASIKIE WENYEWE
Baada ya kupata taarifa hizo, waandishi wetu waliwatafuta baadhi ya wasanii wa kiume Bongo wanaotesa na kuwauliza kuhusu ishu hiyo (wasanii hao hawamo kwenye orodha tuliyonayo).
Wa kwanza kuzungumza alikuwa ni Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni ambaye alisema: “Miye sina la kusema kuhusu hilo, ni vyema kama utamtafuta mwenyekiti (Bongo Movie Unity, Steve Nyerere) ndiye mwenye mamlaka ya kuzungumza masuala kama hayo.”
KULWA KIKUMBA ‘DUDE’
“Hilo suala la ushoga ndani ya Bongo Muvi lipo hata miye nalisikiasikia, lakini halina uthibitisho ila kusemwa linasemwa sana.”
STEVE NYERERE
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’: “Ni kweli taarifa hizo zipo, wasanii wakishakunywa pombe huwa wanafanya mambo ya ajabu sana kuashiria tabia zao halisi, mimi kama mwenyekiti wa Bongo Movie huwa ninaumia sana.
“Nitahakikisha nawafukuza mashoga wote hata kama tutabaki wawili katika kundi letu, bora wawe na heshima.”
MWAKIFWAMBA SASA
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba: “Hiyo ishu ni kweli ipo, ndani ya Bongo Muvi, mashoga wapo wengi sana, ila bado hatujapata ushahidi wa kuweza kuwataka hadharani.”
CHANZO NI GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate