BADO MUAFAKA! Ndivyo ilivyojidhihirisha jana kwenye
Bunge Maalum la Katiba, ambalo limeshindwa kufikia makubaliano ya kura
gani, itumike wakati wa kupitisha uamuzi wa ibara za rasimu ya Katiba
mpya.
Kura inayobishaniwa na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ni
kama iwe ya siri au wazi, jambo lililogawa Bunge hilo katika makundi
mawili, yanayotofautiana kuhusu namna gani uamuzi ufanyike ndani ya
Bunge hilo.
Kutokana
na jambo hilo kushindwa kupata muafaka, kuhusu aina ya upigaji kura
kwenye kufanya uamuzi, sasa Bunge hilo limeamua kupitisha rasimu ya
Kanuni huku kifungu hicho cha kufanya uamuzi, kikieleza tu kuwa uamuzi
utafanywa kwa kupiga kura.
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu,
Pandu Ameir Kificho, alitangaza hatua hiyo jana, baada ya Mwenyekiti wa
Kamati ya Kanuni, Profesa Costa Mahalu, kuliambia Bunge hilo kuwa
kifungu hicho, sasa kitasomeka tu kwamba uamuzi wake, utafanywa kwa
kupiga kura.
Kificho ambaye aliingia ukumbini saa 6.15 mchana
badala ya saa tano aliyoahidi siku ya Jumamosi, aliomba radhi kuchelewa
kwa vile alikuwa anaendelea kushauriana na Kamati ya Kumshauri kuhusu
kanuni, ambayo ilikuwa inaendelea kufanya marekebisho ya kanuni hasa kwa
Kanuni ya 37 na 38.
Profesa Mahalu aliliambia Bunge hilo, kuwa wamekamilisha kazi katika kanuni hizo za 37 na 38, ambazo zinaeleza namna ya kufanya uamuzi utakuwa ni kupiga siri ambayo itaamriwa na Bunge hilo. Kamati hiyo ambayo awali ilipendekeza kura iwe ya siri, sasa imesema tu kuwa mambo yote yataamriwa kwa kura.
Profesa Mahalu aliliambia Bunge hilo, kuwa wamekamilisha kazi katika kanuni hizo za 37 na 38, ambazo zinaeleza namna ya kufanya uamuzi utakuwa ni kupiga siri ambayo itaamriwa na Bunge hilo. Kamati hiyo ambayo awali ilipendekeza kura iwe ya siri, sasa imesema tu kuwa mambo yote yataamriwa kwa kura.
Kwa hatua hiyo ya
Kamati ya Kanuni, ni wazi kuwa uamuzi wa namna gani litafikia maamuzi
umewekwa kiporo. Kificho katika maamuzi yake, alisema kuwa Bunge
lingepitisha kanuni, ambazo zimesharidhiwa kwenye semina hiyo na hizo
mbili bado zitatafutiwa ufumbuzi na Kamati ya Maridhiano.
Tangazo hilo la Kificho lilizua mjadala mkubwa, hali iliyoonesha baadhi ya wajumbe kutokubaliana na hatua hiyo, ambao baadhi yao walitaka Bunge hilo lipige kura ya kumaliza suala hilo na sio kuendelea kuliweka kiporo, kama alivyotaka Mwenyekiti wa Muda.
Tangazo hilo la Kificho lilizua mjadala mkubwa, hali iliyoonesha baadhi ya wajumbe kutokubaliana na hatua hiyo, ambao baadhi yao walitaka Bunge hilo lipige kura ya kumaliza suala hilo na sio kuendelea kuliweka kiporo, kama alivyotaka Mwenyekiti wa Muda.
Wengine wakapendekeza Bunge livunjwe.
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila alisema kwa kuwa wabunge
wanaendelea kutafuna posho, ambayo ni kodi ya wananchi, lakini
wameshindwa kupata muafaka wa jambo hilo, ni vyema Bunge hilo livunjwe
na waletwe watu wengine, wenye dhamira safi ya kufanya kazi hiyo.
“Tangu
tuanze hapa tunavutana juu ya jambo hili na kanuni hapa zimekwama na
hakuna uamuzi mbadala, kama jioni tukija hapa jambo hili bado halijapata
muafaka, ni vyema Bunge hili livunjwe maana hatuwezi kuendelea kupata
posho wakati kazi hazifanyiki,” alisema Kafulila.
Kificho alimjibu
mbunge huyo kuwa Bunge hilo, limeanza kwa tangazo la Rais ;na Rais
ndiye mwenye mamlaka ya kulivunja ;na sio vinginevyo. Hezekiah Oluoch
alisema kwa kuwa Kamati ya Maridhiano, imekutana kwa siku tatu na
imeshindwa kupata ufumbuzi ni bora suala hilo lipigiwe kura.
“Naomba Sekretarieti itugawie karatasi tuamue jambo hili, wewe tulikuchagua kwa siri na suala hili tutalipiga kwa siri,” alisema.
“Naomba Sekretarieti itugawie karatasi tuamue jambo hili, wewe tulikuchagua kwa siri na suala hili tutalipiga kwa siri,” alisema.
Hoja ya Oluoch
ilikuwa kuwa Bunge haliwezi kuendelea na kazi yake ya kuridhia kanuni
nusu, wakati vifungu vingine havijafikia na kumtaka Mwenyekiti atendee
haki Bunge hilo ili vifungu hivyo viwili, vipitishwe na wabunge wenyewe.
Diana
Chilolo ambaye ni Mbunge wa CCM Viti Maalumu, alisema kama ni kura
inapigwa kuhusu vifungu hivyo, ipigwe kura ya wazi. “Kwa nini tunapata
kigugumizi juu ya jambo hili? Kama Kamati ya Mashauriano imekwama kupata
muafaka tupige kura na wananchi wanataka kura iwe ya wazi.”
Mbunge
huyo ambaye wakati anatoa hoja hiyo, alikuwa akizomewa alisema; “
Kuzomea sio jambo la busara na ni tabia mbaya na Mungu hataki, hivyo
mimi nashauri tupige kura ya wazi kuhusu vifungu hivyo”.
William
Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema kwa
kuwa vimebaki vifungu viwili ni vyema Bunge hilo, liendelee na ratiba
yake na hizo kanuni kiporo zitapitishwa baadaye baada ya Kuunda Kamati
ya Kanuni za Bunge.
Hoja hiyo ya Lukuvi, pia ilisababisha azomewe,
lakini akawa ngangari na kuendelea kusema “Nyie zomeeni… lakini mimi ni
sugu wa kuzomewa, hapa ninachokisema ni kwamba kama mnataka semina hii
tumalize kila jambo basi hakuna hata haja ya kuunda Kamati ya Kanuni ya
Kudumu.
“Tusijidanganye kuwa hizi kanuni zitakuwa kamili kwa uhai
wote wa Bunge hili, kuna mambo yanaweza kuletwa hapa kwa ajili ya
marekebisho na ndio maana kunaundwa Kamati ya Kanuni; hivyo suala hili
baadaye litaletwa na kamati hii ni vyema kwa sasa tuendelee na mambo
mengine,” alisema Lukuvi.
Lukuvi alisema sio jambo jema kupiga kura kuamua jambo hilo kwani litagawa Bunge hilo.
Lukuvi alisema sio jambo jema kupiga kura kuamua jambo hilo kwani litagawa Bunge hilo.
“Hata
tukipiga kura hapa kuna kundi litashinda na lingine litashindwa, iweje
tuwe na Bunge ambalo limegawanyika kwenye mambo ya Katiba? Mjumbe wa
Kamati ya Kanuni, George Simbachawene, alimkosoa Lukuvi na Kificho kuwa
vifungu hivyo, haviwekwi pembeni, bali kanuni zitakazopitishwa
zitahusisha vifungu hivyo viwili, kwani vinatamka kuwa uamuzi utafanyika
kwa kura, ila haielezi aina ya kura itakayopigwa.
“Vifungu hivi
havitaji siri au wazi, ila vinasema tutaamua kwa kura, tumefikia hapo
maana wananchi wanalalamika tunakula posho bila kazi, ni vyema tuanze
kazi kwa kuapisha watu na kuchagua Mwenyekiti na twende kwenye kamati.
“Tutakapofikia
wakati wa kutoa uamuzi kila mtu atakuwa ameshajiuliza na Kamati ya
Kanuni italeta jambo hilo na sisi kama Bunge tutaamua ni aina gani ya
kura ipigwe na wakati huo, Kamati ya Maridhiano naamini itakuwa imefikia
hatua nzuri,” alisema Simbachawene.
Baada ya maoni hayo ya Simbachawene, wajumbe wengi walisimama kutaka kutoa maoni, lakini Kificho alisema kuwa kilichofikiwa kwenye Kamati ya Kanuni, ndicho mbacho kimeamriwa kwenye Kamati ya Mashauriano hivyo ni vyema jioni wapitishe kanuni hizo.
Baada ya maoni hayo ya Simbachawene, wajumbe wengi walisimama kutaka kutoa maoni, lakini Kificho alisema kuwa kilichofikiwa kwenye Kamati ya Kanuni, ndicho mbacho kimeamriwa kwenye Kamati ya Mashauriano hivyo ni vyema jioni wapitishe kanuni hizo.
Maoni ya Wabunge Wakizungumza nje ya ukumbi
wa Bunge, Joseph Selasini, alisema makundi ya kisiasa, yamelivuruga
Bunge na yamevuruga maridhiano ndani ya Kamati ya Mashauriano. Alishauri
kwamba kuna haja ya kuongeza watu kwenye kamati hiyo ili kufikia
muafaka wa jambo hilo.
“Kamati ya Maridhiano ikaonane na Rais
Jakaya Kikwete ili kupata ushauri na hatimaye kufikia uamuzi kuhusu
vifungu hivyo. Haiwezekani kupitishwa rasimu ya kanuni wakati vifungu
vya 37 na 38 havijafanyiwa uamuzi, lazima uamuzi ufanyike leo na kama
tunakwepa leo tutaweza lini?” Alihoji Selasini.
Murtaza Mangunga
alitaka Kamati ya Mashauriano, iendelee kufanyia kazi vifungu hivyo na
wajumbe wa Bunge la Katiba waendelee na shughuli nyingine kujadili na
kupitisha rasimu ya Katiba.
Dk Henry Shekifu alisema busara
imetumika kwa vile imeshindikana kupata ufumbuzi, ni vyema Bunge
liendelee na mambo mengine na baadaye watatafuta namna nzuri ya kufanya
uamuzi wa kupiga kura.
“Kwa nini tugome kuendelea na kazi zingine
hadi suala hilo lipata ufumbuzi? Hivi wananchi watatuelewaje hii
inaonesha watu wana nia mbaya na jambo hili,” alisema Dk Shikifu.
Profesa Ibrahim Lipumba alisema alichofanya Mwenyekiti wa Muda wa Bunge, ni kulaza matatizo kwani Bunge haliwezi kuendelea kujadili Katiba wakati kanuni zenyewe hazijakamilika na inaweza kuleta matatizo huko mbele ya safari.
Profesa Ibrahim Lipumba alisema alichofanya Mwenyekiti wa Muda wa Bunge, ni kulaza matatizo kwani Bunge haliwezi kuendelea kujadili Katiba wakati kanuni zenyewe hazijakamilika na inaweza kuleta matatizo huko mbele ya safari.
Lipumba alisema kwenye Kamati ya Mashauriano,
walikubaliana kuwa kuwepo na kura ya siri na ya wazi, kwa mambo ya
kawaida iwe wazi; lakini kwenye mambo nyeti kama ya dini na Muungano,
ambayo yanahatarisha maisha ya wajumbe ipigwe kura ya siri.
“Tulikubaliana
hivyo, wenzetu wajumbe wa CCM walivyoenda huko wakatugeuka, tuliwataka
pia wakashauriane na Mwenyekiti wao, lakini leo hatukukutana badala yake
tumekuja bungeni na hili ndilo ambalo limetokea,” alisema.
Profesa
Lipumba alisema huwezi kuendelea mbele na mijadala ya Katiba wakati
utaratibu wa kufanya uamuzi haujulikani, kwani wajumbe watafanya
mijadala na ikifika wakati wa kupiga kura itashindikana kwani kanuni
imekaa kimya juu ya suala hilo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe, ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Mashauriano, alipinga agizo la
Kificho la kupitisha kanuni hizo bila kuwepo maridhiano.
Alisisitiza
kuwa hakuna afya kwa Bunge hilo kuamua mambo yake kwa kupiga kura ya
siri au ya wazi. Alisema mchakato wa Katiba ni wa maridhiano na sio wa
kupiga kura kwa kupata shinikizo kutoka kwenye makundi ya vyama vya
siasa. “
“Hapa ikipigwa kura CCM ikashinda wengine watagoma na
upande mwingine ukishinda CCM nao watagoma, hivyo hatapatikana mshindi
na utakuwa mwisho wa mchakato wa Katiba,” alisema. Alisema baadhi ya
wajumbe wa Bunge hilo, wanapata shinikizo na maelekezo ya vyama vyao nje
ya maelekezo ya kifungu cha nne cha kanuni hizo, ambacho kinapiga
marufuku wajumbe wa Bunge hilo kupata shinikizo lolote nje ya dhamira
yake. Alisisitiza kuwa kura ya siri au ya ndio, italivunja Bunge na
amependekeza maridhiano zaidi yatumike.
Alitoa mfano kuwa kura ya
wazi kwa mambo ya dini au Muungano, yanawaweka baadhi ya wajumbe katika
hatari kubwa ya maisha yao. “Kuna suala la Muungano hapa, Mzanzibari
akipiga kura ya wazi misimamo ya huko mnaifahamu anaweza kumwagiwa
tindikali na hata nyumba yake kuchomwa, lakini pia kuna misimamo ya dini
ni hatari kwa muumini mwenyewe,” alisema Mbowe.
Mchungaji
Christopher Mtikila, kwa upande wake, alisema kwamba alichofanya
Mwenyekiti wa Muda ni kuahirisha tatizo. Alisema kuwa ushabiki ambao
umeoneshwa kwenye mambo ya msingi, unaweza kuvuruga upatikanaji wa
Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Felix Mkosamali,
ambaye ni Mbunge wa Muhambwe alikosa uvumilivu baada ya kuitwa mtoto na
kusababisha majibizano ya ‘matusi’ miongoni mwa wajumbe.
Majira ya saa 10 jioni baada ya Mwenyekiti wa Muda, Pandu Ameir Kificho kufungua Bunge, Mkosamali alisimama kuomba muongozo, lakini aliambiwa asubiri na atapewa nafasi wajumbe wa Bunge hilo wakifika nusu yake.
Majira ya saa 10 jioni baada ya Mwenyekiti wa Muda, Pandu Ameir Kificho kufungua Bunge, Mkosamali alisimama kuomba muongozo, lakini aliambiwa asubiri na atapewa nafasi wajumbe wa Bunge hilo wakifika nusu yake.
Hata
hivyo, baada ya dakika kadhaa, James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa
Chama cha NCCR Mageuzi, chama anachotoka Mkosamali, alisimama na kuomba
muongozo.
Alipokubaliwa alisema kutokana na kutopata nakala ya
Rasimu ya Kanuni, hawataweza kujadili rasimu hiyo na Kificho, akamuambia
ndiyo maana amesimamisha Bunge kwa muda ili nakala wapewe wajumbe.
Kutokana
na hatua hiyo, Mkosamali alisimama na kusema; “Mwenyekiti samahani
nakuheshimu sana lakini mimi umeninyima nafasi ya kuzungumza lakini
mjumbe (Mbatia), umempa nafasi hivi sivyo njia sahihi ya kuendesha
Bunge.”
Baada ya kumaliza, ikasikika sauti ya mbunge mwanamke,
ikamjibu “mtoto mdogo hana adabu” na alipomaliza ikatokea sauti nyingine
ya Mbunge mwanamume, akajibu “Kubwa jinga halina adabu.”
Naye Mkosamali akajibu; “hakuna mtoto mdogo aliyeishinda CCM.” Kutokana na malumbano hayo, yaliyodumu kwa dakika tano, Kificho akasema; “hakuna mtoto hapa watu wote ni wajumbe”.
Alipomaliza kutoa kauli hiyo, Kificho akaahirisha Bunge saa 10:27 jioni hadi saa 12:00 jioni, kutokana na kazi ya kudurufu kanuni kutomalizika na kupewa wajumbe ili waendelee kuziridhia.
Naye Mkosamali akajibu; “hakuna mtoto mdogo aliyeishinda CCM.” Kutokana na malumbano hayo, yaliyodumu kwa dakika tano, Kificho akasema; “hakuna mtoto hapa watu wote ni wajumbe”.
Alipomaliza kutoa kauli hiyo, Kificho akaahirisha Bunge saa 10:27 jioni hadi saa 12:00 jioni, kutokana na kazi ya kudurufu kanuni kutomalizika na kupewa wajumbe ili waendelee kuziridhia.
CHANZO NI HABARI LEO
No comments:
Post a Comment