Katibu
mkuu wa CCM Mkoa wa Iringa,Ndugu Hassani Mtenga akizungumza na
wanahabari wa Iringa katika ofisi za chama hicho mapema leo.
Katibu
mkuu wa CCM Mkoa wa Iringa,Ndugu Hassani Mtenga akizungumza na
wanahabari wa Iringa katika ofisi za chama hicho mapema leo.
Sahihi halali ya Mwigulu Nchemba ambayo iko tofauti ya waraka uliosambazwa.
======= ====== ========
Na Denis Mlowe,Iringa
KATIBU wa CCM Mkoa wa Iringa Hassani Mtenga amekanusha chama hicho
kuhusishwa na waraka aliodai umesambazwa na Chadema ukihusu mchanganuo
wa matumizi ya Sh Milioni 560 katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga.
Alisema propaganda
za kisiasa za wapinzani ndio chanzo cha waraka huo kusambaa na
kuwaonyesha waandishi wa habari sahihi kamili ya Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Mwigulu Nchemba anayesemekana alisaini waraka huo.
"Kwanza
kuna kosa hawa wenzetu wanafanya, waraka huo una anwani ya Katibu wa
CCM Mkoa wa Iringa lakini chini unaonekana umesainiwa na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba, sahihi ambayo imegushiwa,” alisema Mtenga
Katika
waraka huo wenye kichwa cha habari kinachosema ‘Malipo ya kamati
mbalimbali kwenye ushindi wa jimbo la Kalenga, umeidhinisha fedha hizo
zitolewe kwa viongozi mbalimbali kama walivyoomba oili zitumike katika
kampeni za jimbo.
Waraka
huo unaonyesha kuwa CCM wametumia kiasi cha shilingi milioni 560 kwa
ajili ya timu ya ushindi wiki hii ya mwisho ya kampeni, fedha hizo
zimetumwa kutokana na tathimini yenu kuwa ni hali mbaya kwetu kwa barua
yenu yenye kumb Namba CCM/IR/VOL11/096.
“Hakikisha
kiwango hiki kinwafikia walengwa wote wafuatao kwa uwiao
tuliokubaliana kulingana na maeneo yao na wao wazigawe kwa mabalozi wetu
kwenye kila kitongoji na kata apewe Balozi Sh850,000, Mama Galinoma Sh
Milioni 80, Mama Ray (Ulanda) Sh Milioni 60, wenyeviti wa kata wa CCM
kila mmoja Sh Milioni 20, makatibu wa kata kila mmoja Sh Milioni 8,
makatibu wenezi CCM kila mmoja Sh Milioni 14 na Kamati ya ushindi Nzihi
Sh Milioni 108,” sehemu ya waraka huo inasema.
Mtenga
alisema lengo la kusambazwa kwa waraka huo lilikuwa kuwaaminisha wapiga
kura wa Kalenga kwamba kuna fedha zimetolewa na CCM kwa ajili yao
lakini zimeliwa na watu wanaotajwa katika waraka huo.
Alisema
kuna kila dalili kwamba waraka huo uliandaliwa na Chadema kwa lengo la
kuwarubuni wananchi wa jimbo la Kalenga wakose imani na CCM.
Wakati
huo huo CCM kimempa siku 7 Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Iringa, OCD
Sifael Pyuza kuwataka radhi kwa madai ya kuwadhalilisha katika ofisi za
chama hicho mkoani hapa baada ya kuwafanyia uchunguzi bila kuwa na
kibali maalum.
Kamanda
Pyuza anatuhumiwa na chama hicho kukihusisha na mchezo mchafu wa siasa
kwa kuficha watu ndani ya jengo la ofisi yake waliokuja katika uchaguzi
mdogo wa Kalenga uliofanyika machi 16 na ccm kuibuka kidedea.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliyasema hayo jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuwa , Machi 16 mwaka
huu kamanda huyo alituma makechero wa jeshi hilo katika ofisi za CCM za
mkoa wa Iringa waliotumia mabavu kupekua ofisi moja baada ya nyingine
bila kuwa na kibali halali.
Alimtaka kamanda huyo kuwaomba radhi baada ya tuhuma yake dhidi yao kubainika haina ukweli.
na
chama cha mapinduzi hakiwezi kukaa kimya kwa udhalilishaji huu
uliofanywa na mkuu wa upelelezi wa wilaya kwa sababu jambo hilo ni sawa
na kukiingiza chama cha mapinduzi katika kashfa ya mchezo mchafu wa
kisiasa.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema
hana taarifa yoyote kuhusiana na madai ya chama hicho lakini yupo
tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi.
No comments:
Post a Comment