EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, March 5, 2014

MANGULA AISIMANGA CHADEMA KALENGA, ASEMA CCM LAZIMA ISHINDE‏

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na viongozi wa CCM katika kata ya Mgama kijiji cha Mgama mara baada ya kuwasili kjijini hapo kwa ajili ya kufanya mkutano na wajumbe wa harmashauri kuu ya Kata hiyo ili kujadili kwa pamoja mwennendo wa kampeni katika jimbo la Kalenga ambapo chama hicho kimemsimamisha Bw. Godfrey Mgimwa kuwa mgombea wa jimbo hilo, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 16 mwaka huu. 2 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akishiriki kuimba wimbo na wana CCM mara baada ya kuwasili katika kikao hicho cha ndani kilichofanyika kwenye kijiji cha Mgama. 3 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akishiriki kucheza ngoma kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa ndani uliofanyika leo kwenye kijiji Mgama 4 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akifurahia jambo kwa kupiga makofi wakati wa mkutano huo wa ndani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini mama Delfina Mtavilalu. 
 5 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akizungumza na waandishi wa habari kijijini Mgama mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa ndani. 6 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisoma mambo muhimu yanayohusu uchaguzi huo kwa wana CCM. 7 
Baadhi ya viongozi wa CCM katika ngazi ya vijiji na kata wakiwa katika mkutano huo 8 
Msafara wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula ukiwasili katika kijiji cha Mgama

  9Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa ndani
................................................................................................
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amekifananisha chama cha CHADEMA sawa na wachuuzi wa biashara za mkononi (wamachinga) kwa kutokuwa na maeneo rasmi ya kuendesha shughuli zao. Mangula amesisitiza kuwa CCM imejipanga na ina uhakika wa kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa vijijini. Kiongozi huyo wa juu wa CCM aliyasema hayo jana katika kijiji cha Mugama kata ya Mugama wilayani humo wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya kata hiyo. Mangula alitoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi huo katika kata ya Mugama ambapo Katibu wa CCM kata ya Mugama Sylvester Samon kueleza kuwa chama cha CHADEMA ambacho ni mshindani wa CCM katika uchaguzi huo hakina dalili kushinda. Samson alisema CHADEMA haina ofisi hata moja katika kata nzima ya Mugama jambo linalokitia hofu chama hicho na kulazimika kutumia mbinu chafu ikiwemo kushusha bendera za CCM na kuchana mabango ya mgombea wake. Baada ya kuelezwa hayo, Mangula alisema CHADEMA kimekosa mwelekeo ndani ya kata hiyo na jimbo zima la Kalenga kwa kuwa kimekuwa sawa na wamachinga kwa kutokuwa na na ofisi ambazo ni dalili ya kukubalika na kuwa na wanachama kwenye eneo husika. “CHADEMA hakina hata ofisi moja katika kata nzima, hivi unaweza kusema kina dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwenye eneo hili au wanataka kuwalaghai na kuwarubuni wananchi,” alisema. Alisema CCM imejipanga kupata ushindi wa kishindo kutokana na mafanikio na utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambapo mambo mbalimbali ya maendeleo yamefanikiwa kutekelezwa. Kwa mujibu wa Mangula, uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi ya mbunge wa CCM hivyo ni vyema wana-Kalenga wakamrudisha mwana-CCM ili akamilishe ahadi zilizotolewa na Chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Mugama, Betha Luhavi, alisema Chama kina taarifa kamili kuhusu wapiga kura wa eneo hilo hivyo hakuna mtu kutoka nje ya eneo hilo atakayepewa nafasi ya kujipenyeza ili kuvuruga uchaguzi huo. Betha alisema hadi sasa tayari CCM imefanikiwa kuyazunguukia matawi yote yaliyo kwenye kata hiyo kwa lengo la kuhamasisha makada na wapenzi wake siku ya kupiga kura wajitokeze kupiga kura. Alisema viongozi na wapenzi wa CCM watakuwa mstari wa mbele kuhamasisha amani kipindi chote cha kamepeni na siku ya uchaguzi ili kuhakikisha ubnafanyika kwa amani. Aidha, alisema CCM itashirikiana na vyombo vya dola kufichua uhalifu wa aina yoyote unaolenga kuvuruga uchaguzi na amani katika kata hiyo na jimbo la Kalenga kwa jumla. Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kalenga unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu ambapo CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa kuwa mgombea wake atakaechuana na wagombea wengine. uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake Dk. William Mgimwa kufariki dunia Januari mwaka huu wakati akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA)

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate