Staa
nguli wa muziki wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila’Ray C’amemtaka
aliyekuwa mpenzi wake, Lord Eyez kubadilika kutokana na changamoto za
maisha zinazomkuta hasa ya kutuhumiwa mara kwa mara kuiba mali za watu.
Msanii
huyo wa hip hop kutoka kundi la Weusi,Lord Eyez anashikiliwa na jeshi
la polisi kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa kuvunja gari na kuiba laptop
huko Arusha,ambapo Kundi lake la Weusi limetoa tamko kuhusu msanii huyo
kutoka na natukio hilo.Kupitia
account yake ya Instagram aliandika hivi…Badilika babaa......Nakuombea
sana ujitambue na ubadili mwendo wa Maisha yako...Wewe bado ni kijana
mdogo sana na una kipaji cha pekee.....Kila Mtu Ana changamoto yake ya
maisha,angalia wapi ulipokosea,litambue tatizo halafu kubali kwamba una
tatizo then rekebisha Hilo tatizo.Anza Maisha mapya,Badilika.........Majanga yote yanayokukuta ni ishara tosha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba unakoelekea siko,Kama una akili timamu basi utagundua Hilo na utajirekebisha babaa,Nakuombea kila la kheri katika mabadiliko ya Maisha yako...........Karibu Kwenye Tiba ya Methadone...................Methadone Kiboko ya Madawa.
Kwa mujibu wa Ray C aliwahi kusema kuwa Lord Eyez ndiye mpenzi wake alimuingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya lakini sasa ameshaacha na kuanzisha taasis yake ya Ray C Faundation ya kupiga vita utumiaji wa madawa hayo.
No comments:
Post a Comment