Mamlaka za kipolisi jijini New York, zimethibitisha kuwa watu wawili wamepoteza maisha ndani ya moja ya nyumba vilivyokuwa katika jengo moja la ghorofa ambalo limeanguka leo hii.
Vituo vya habari katika eneo hilo vimetoa ripoti zenye kueleza pia kuwa kuna watu wapatao 11 ambao wameonekana kuwa na majeraha kadhaa kutokana na tukio hilo ambalo wenyeji wa maeneo hayo wameeleza kuwa limetokana na kitu kama mlipuko.
Aidha, kampuni moja ya kutoa huduma za kusambaza gesi katika maeneo hayo, imeamuriwa kufunga huduma zake haraka iwezekanavyo, ili kuepusha majanga zaidi hii ikitokana na ukweli kuwa, kulisikika mlipuko mkubwa toka katika moja ya vyumba kwenye jengo hilo.
Raia mmoja ameeleza kuwa, amekuwa akisikia harufu ya gesi kila alipopita mahali hapo, kwa takriban wiki moja kabla ya tukio hili.
"Tuliona watu wakirushwa kutokea madirishani, hawa walikuwa majirani zangu, na kwa ujumla kishindo kilikuwa kikubwa sana kama bomu vile, na kilitetemesha jengo zima" ameeleza shuhuda mmoja, ambaye aliungwa mkono na shuhuda mwingine alyesema hali haikuwa tofauti na ilivyokuwa wakati wa tukio la kulipuliwa kwa majengo pacha kwenye sakata la September 11.
No comments:
Post a Comment