EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, March 25, 2014

MWAKIFWAMBA: SANAA HAILIPI, WENGI WANAISHI MAISHA YA KUIGIZA!

SOKO la filamu limekua, maisha ya vijana wengi yamebadilika kutokana na sanaa hiyo. Hata hivyo bado kuna changamoto kadhaa; malipo ya wasanii na mikataba mibovu imeendelea kuwa kilio kwao.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba
Hilo linawafanya waendelee kubaki palepale licha ya kupanda kwa hatua nyingi takriban miaka saba iliyopita. Sinema kwa sasa, imebaki kuwa na manufaa zaidi kwa msambazaji badala ya msanii ambaye kimsingi ndiye mhusika mkuu katika utayarishaji.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba amefafanua mengi kuhusu changamoto zilizopo katika sanaa hiyo.

Mwakifwamba alikuwa mgeni wetu katika Live Chumba cha Habari inayoendeshwa na gazeti hili na kuruka hewani katika Global TV Online iliyo ndani ya mtandao wa www.globalpublishers.info
Mwakifwamba alisema:
“Mimi kama rais wa shirikisho ambalo lina vyama kadhaa, siridhishwi na maendeleo ya wasanii wetu.
“Ni kweli sanaa inakubalika sana tofauti na zamani lakini hailipi. Inamnufaisha msambazaji tu. Wasanii wengi wakiulizwa kwenye vyombo vya habari wanasema inalipa.
Ni waongo. Wengi wanaishi maisha ya kuigiza.
“Wasanii wanauza haki zao. Kuuza filamu kwa mkataba wa moja kwa moja ni kuuza haki.
Kinachowasumbua wasanii wetu ni njaa. Mfano mimi, naweza kutoa filamu yangu, lakini kwa sababu soko si zuri ndiyo maana sitoi. Siwezi kuuza haki yangu.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba akiongea na wanahabari wa Global (hawapo pichani).
“Lakini wakati wa ukombozi unakuja. Muda ukifika hakuna atakayeweza kuzuia. Tutatetea haki za wasanii kwa sababu tunajua tutakuwa tumesaidia vizazi vyetu vijavyo. Wasanii waache uongo ili wasaidiwe.
“Utakuta mtu anaonekana anaendesha gari zuri mitaani, chunguza, siyo lake. Ameazima. Wanalazimisha maisha ya kuonekana bora lakini ndani ya mioyo yao wanavuja damu.”
KWA NINI WASANII HAWAFANIKIWI?
“Kuna mambo mengi lakini kwanza, serikali inapaswa kuitambua sanaa kama sekta rasmi ya ajira. Itambue na kulinda haki za wasanii wetu. Mpaka sasa, serikali imetamka kuwa inalinda mali zinazohamishika na zisizohamishika.
“Hapo ndipo kwenye tatizo, msanii mali yake haipo katika makundi yote hayo. Ni mali ya ubunifu. Ipo kichwani. Sheria ya Tanzania inatakiwa kuanza kutambua haki ya msanii, hapo ndipo tutakapoanza kuona mafanikio ya jasho letu, vinginevyo tutaendelea kubaki palepale miaka nenda rudi.
“Dunia inaongozwa na akili, lazima akili nayo itambulike kwenye sheria za nchi yetu. Hivi kweli serikali haioni mchango wa wasanii katika kuongeza ajira? Filamu moja mpaka imfikie mteja, inakuwa imeshapita maeneo mengi sana.
“Kwanza kuna mtu wa kutafuta location (mandhari), mapambo, muongozaji, mtu wa sauti, taa, wasanii, graphics, editing (uhariri), mtengeneza kava na mwisho msambazaji. Wangapi hapo wamepata ajira? Serikali itutambue, ituweke kwenye katiba ya nchi, sheria itamke kuhusu haki zetu.”
SKENDO KWA WASANII VIPI?
“Nakemea  wasanii kufanya mambo yasiyofaa mbele ya jamii. Lakini lipo tatizo moja... unajua mimi nipo kwenye sanaa mwaka wa 28 sasa, nina uzoefu wa kutosha.
“Siku hizi mambo yamebadilika. Zamani wasanii tulikuwa tunalelewa kwenye makundi, tulikuwa na wazee wetu ambao walisimamia nidhamu
“Sasa hao ambao wanaokotwa huko barabarani kwa sababu ya uzuri ndiyo wanaokuja kuharibu sanaa. Watayarishaji wabadilike. Siyo kila miss ni msanii. Siyo kila msichana mzuri anaweza kuigiza. Wazingatie weledi, siyo mwonekano.”
BIFU NA BONGO MUVI VIPI?
“Bifu la nini? Mimi ni baba, wao ni watoto. Kwanza sikia... wale siyo wanachama wangu. Nawashauri wajiunge kwenye vyama vyangu ili niwatambue kama sehemu ya shirikisho.
“Unajua wale wanaongozwa na ustaa. Wanaamini ustaa upo juu ya sheria, siyo kweli. Mimi naamini katika uelewa na uwezo.
Isitoshe mtu wa kwanza aliyetoa wazo la Bongo Muvi ni mimi.
“Nakumbuka nilikuwa mimi, Dude (Kulwa Kikumba), William na Ruge Mutahaba, tukaunda Bongo Muvi ili tucheze mechi na Bongo Fleva kwa ajili ya kuchangisha fedha za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto.
“Tulifanikiwa sana. Hapo sasa walafi wachache wakalazimisha wasanii waende Mwanza wakacheze mechi nyingine ili wapate fedha, nikakataa hilo wazo, ndiyo mwanzo wa kutengana nao. Niwaambie tu Watanzania, chombo mama cha wasanii wa filamu nchini ni TAFF, si vinginevyo.
“Kwanza Bongo Muvi si chama kama wengi wanavyofikiri, ni kampuni na ina wamiliki wake tisa, hao wengine wanafuata mkumbo kwa sababu hawajitambui. Kama wanabisha, waonyeshe usajili wao wa Basata, maana chombo pekee kinachosajili kazi za wasanii ni Basata.”
WASANII WAKIUGUA HUOMBA MISAADA, TAFF HAINA UWEZO WA KUWASAIDIA?
“Ndiyo maana napenda sana maneno; uelewa na uwezo. Nimeshapiga kelele, wasanii tujiunge kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ‘NSSF’, wengi hawataki.
“Kuna mmoja alifikia hatua akaniambia, yeye anaweza kupitisha hata miaka mitatu bila kuugua, ana sababu gani ya kulipia NSSF? Huyu mtu anafikiria vizuri kweli
"Nilizungumza na NSSF, wamekubali wasanii wawe wanachangia shilingi 20,000 tu kwa mwezi, ambapo ataweza kupata matibabu bure yeye, mume/mke na watoto wanne.
Jambo la kufurahisha zaidi, NSSF wamesema, kwa sababu sisi ni wasanii, ukichanga kwa miaka mitatu mfululizo unaweza kukopeshwa nyumba kwa masharti nafuu na ukalipia kwa miaka 15 – hawataki.
“Hapo sasa utaona ni kwa namna gani wasanii wetu wanaamini katika ustaa.
TAFF haiwezi kumsaidia msanii mmoja mmoja ila inashauri, kutafuta na  kuonyesha njia za namna ya kutatua matatizo ya wasanii.” 

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate