Katika
kuelekea siku ya wanawake duniani,iliyoadhimishwa Duniani kote mnamo
Machi 5, kampeni ya Grow ikiongozana na mmoja wa mabalozi wake muigizaji
Jacob Stephen ‘JB’ iliungana na kipindi cha EATV Nirvana na kuutembelea
mji wa Lushoto,Jijini Tanga.
Kampeni
ya GROW, inayoendeshwa na Oxfam, inahamasisha mabadiliko kwenye mifumo
iliyopo ili iwafanufaishe wakulima na wafugaji/wavuvi wadogo wadogo
hususani wanawake wawe na maisha endelevu! Inawasherekea kwa mchango wao
mkubwa wa kulisha nchi huku wakipambana na changamoto nyingi ikiwemo
ukosefu wa masoko, pembejeo na miundo mbinu. Katika harakati hizi, mnamo
mwaka 2011, shindano la "Mama Shujaa wa Chakula " lilizinduliwa rasmi
hapa nchini. Lengo la tuzo hii ni kutambua mchango wa wanawake hasa
waishio vijijini.
Huko Lushoto hali ilikuwa kama picha zinavyoonyesha...
Alfajiri
ya Machi 6, timu ya Nirvana, Grow, pamoja na JB walielekea soko kuu la
Lushoto ambapo walikutana na wakulima ili kusikia hadithi zao za
mafanikio pamoja na changamoto. Nirvana na Kampeni ya GROW wanahamasisha
lifestyle njema! Lakini tunavyokula vyakula bora, vyenye virutubisho
tunajua vinatoka wapi!
Akizungumza
kutoka katika sehemu yake ya biashara, Zinira Ally (kushoto aliyekaa)
alishuhudia jinsi ambavyo anasomesha watoto na kulisha familia yake kwa
pesa inayotokana na biashara yake ya uuzaji wa mbogamboga na matunda.
"Nzenze"... Salaam na wapenzi wa filamu zikiendelea.
JB, Lotus na Deo wakitizama mazao mbalimbali katika soko kuu la Lushoto.
Veronica
Joseph ambaye ni muuzaji wa mboga mboga sokoni Lushoto anasema
angependa kuona mabadiliko katika miundombinu ya soko ili kulinda ubora
wa mazao, “soko halina ubora, watu wananunua vyakula hivi hivi kwa bei
ghali kwenye supermarket kwa sababu ya ubora, sie tunauza tu bora
tunauza, tunaogopa vyakula kuoza, tungekuwa na mafriji ya kuhifadhia
mboga mboga na sisi tungeweza kuuza bei sawa na supermarket.”Akiendelea
kutaja changamoto, Veronica ambaye ni mama wa watoto wawili, alionyesha
kusikitishwa kwake na maisha duni wanayoishi wakulima, “mkulima analima
chakula ambacho wengine wanakula hadi kutupa lakini yeye hawezi hata
kula mlo kamili kwa sababu kipato anachopata ni kidogo”
Veronica anaamini kama, “masoko yangeboreshwa, tungeuza bidhaa kwa bei
nzuri ili na sisi tusomeshe watoto wetu na kujikimu kimaisha.”
Uvuvi unalipa..??
Ugeni
umefika katika meza ya Asha Paulo (Kushoto) na Shakira Rashid (kulia),
hawa ni wauzaji wa samaki katika soko kuu la Lushoto. Asha na Shakira
wanaelezea jinsi ambavyo mikopo kwa wakulima na wafugaji isivyokuwa
rafiki. Asha anasema, “mikopo ina masharti makali sana, sidhani kama
inamlenga mtu wa hali ya chini kwani makato ni makubwa sana.”
Watangazaji
wa kipindi cha Nirvana, Lotus na Deo walishangaa kuona apple
zinazolimwa Tanzania. Kisado kimoja ambacho kwa wastani kina ma-apple
ishirini (20) kinauzwa kwa Tshs. 2000 wakati kwa wastani apple moja
jijini Dar es salaam linauzwa hadi Tshs. 1000. Baada ya kuonja, Deo
anashangaa kuona ladha haipishani sana na ile ya matunda hayo
yanayoagizwa kutoka nje.
Ukweli ni kwamba miundo mbinu, technolojia, sera na mifumo iliyopo
imewaangusha wakulima hapa Tanzania!
Fikiria kwamba ni rahisi na kuna faida zaidi kusafirisha apple kutoka
nje ya nchi kuliko hapa hapa Lushoto Tanzania!
Paulina
Isaya (mwenye nguo nyeusi), muuzaji wa matunda apple katika soko kuu la
Lushoto anasema, “kama wakulima wangepewa mafunzo sahihi, mbegu bora na
kuhakikishiwa masoko, hakika matunda hayo yangekuwa na kiwango kama
hayo yanayoagizwa kutoka nje”.
Taswira ya soko kuu la Lushoto kwa nje.
JB akiangalia kabichi zilizowekwa pembezoni mwa barabara. (Haikujulikana mara moja kama zilikuwa zinasubiri kusafirishwa ama la)
No comments:
Post a Comment