Kweli Urais hauna ubia wala muda ama sehemu
ya kuchapa kazi. Wakati wowote na mahali popote ni sehemu ya kazi, kama
inavyoonekana hapa ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametulia ndani ya ndege akisafiri
kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma huku akiifanyia kazi hotuba yake
ambayo ataitoa katika Kikao cha Bunge Maalum la Katiba, Ijumaa, Machi
21, 2014.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia Bunge Maalum la Katiba kwa
mujibu wa Kanuni 7(1)g na Kanuni 75(1) la ya Kanuni za Bunge Maalum.
PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment