MWENYEKITI wa kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amenaswa akipiga msosi wa maana.
Katika pitapita za hapa na pale, kamera
yetu ilimnasa Steve maeneo ya Sinza katika hoteli maarufu ya Shamool
akila msosi wa maana na alipohojiwa alidai kuwa ameshazoea kula kwenye
hoteli zenye hadhi kwani anaogopa uswahilini atanaswa na mapaparazi.
Steve baada ya kunaswa na paparazi wetu.
“Unajua mtu ukishakuwa maarufu unaogopa hata kula kwa mama lishe kwa
sababu waandishi wakikunasa wanaenda kukuandika tu hata mtaani watu
wanabaki wakikushangaa ndiyo maana nimekuja kula hapa,”alisema Steve.
(Picha na Gladness Mallya / GPL)
No comments:
Post a Comment