Huyu
ndiye mama mkubwa wa mtoto Adolotea Nyavike, Bi. Salome Kiegu
(35) ambaye alitoweka na mtoto huyo kusikojulikana huku wasamalia wema
wakitaka kutoa misaada.
Hatimaye mama aliyetoroka na mtoto
aliyeungua moto apatikana baada ya kupiga simu Mbeya yetu Blog kuwa yupo
Njombe kwa baba mzazi wa mtoto huyo na kuomba radhi kuwa aliondoka bila
kuaga na leo saa nane mchana atakuwa amerudi na mtoto huyo.
Mama huyo amejitokeza baada ya mtandao wa Mbeya Yetu kuandika mapema jana kwamba alikuwa
ametoweka bila taarifa zozote. Akiongea na Mbeya Yetu Blog amedai
kwamba yeye aliondoka ili akashauriane na wazazi wa mtoto huyo ili waone
ni jinsi gani watamsaidia lakini alipohojiwa amejikanyaga kanyaga na
kuongea bila kuwa na uhakika na kile anachozungumza.
Hata hivyo baadaye atafanyiwa mahojiano ya kina na kuona ukweli uko wapi kwa kuwa anatia
mashaka na maelezo yake. Tunaendelea kusisitiza kuwa kama kuna mtu anahitaji kumchangia mtoto huyo asifanye hivyo kwa kuwa mama huyo ameonesha wasiwasi na kuondoa imani watu.
mashaka na maelezo yake. Tunaendelea kusisitiza kuwa kama kuna mtu anahitaji kumchangia mtoto huyo asifanye hivyo kwa kuwa mama huyo ameonesha wasiwasi na kuondoa imani watu.
(Chanzo: Mbeya Yetu Blog)
No comments:
Post a Comment