Katibu
Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bibi. Anna T.
Maembe akisisita haja na umuhimu wa wazazi kuwawezesha watoto wao wa
kike kuyapenda masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu ( STEM)
badala ya kuliachia jukumu hilo serikali au walimu. Alikuwa akizungumza
katika mkutano wa pembezoni ulioandaliwa kwa pamoja kati ya Tanzania,
Uingereza na Kampuni ya Kimataifa ya GlaxoSmithkline ili kujadili fursa
na changamoto za mwanafunzi wa kike katika masomo hayo, kulia kwa Katibu
Mkuu ni Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bibi. Irina Bokova ambaye alikuwa
modereta wa majadiliano hayo na pia alielezea nafasi na Mchango wa
UNESCO katika kumsaidia mtoto wa kike. Kushoto ni Balozi Ramadhan Mwinyi
, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Waziri
wa Wizara ya Wanawake na Usawa wa Uingereza, Bibi, Maria Miller ( Mb)
akielezea uzoefu wa nchi yake katika kuwahamasisha watoto wa kike
kupenda masomo ya STEM, kulia kwake ni Bibi Nicola Yates, Makamu wa Rais
wa UK and Ireland Phamarceuticals na Meneja Mkuu wa GlaxoSmithkline.
Nyuma ya Waziri Miller na anayefuatilia kwa makini majadiliano hayo ni
Mwanamitindo Bi. Flaviana Matata ambaye pamoja na kujikita fani ya
mitindo na ambayo imemjengea heshima kubwa, lakini pia kupitia Taasisi
yake ya Flaviana Matata Foundation ameonyesha mapenzi makubwa ya
kuwasaidia wanafunzi kuipenda shule na kudumu shuleni.
Makatibu
Wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bibi. Asha Ali Abdullah (
Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto) na
Bibi. Mwanaidi Salehe Abdulla ( Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amari)
wakifuatilia majadiliano hayo kuhusu fursa na uwezeshaji wa wanafunzi wa
kike kujiunga na masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu.
sehemu
wa washiriki wa Mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake,
walioshiriki majadiliano hayo ambapo pia walipata fursa ya kuchangia kwa
kuuliza maswali meza kuu iliyowahusisha Katibu Mkuu, Anna Maembe,
Mkurugenzi Mkuu UNESCO, Irina Bokova, Waziri Maria Miller ( Mb) na
Nicola Yates Meneja Mkuu GlaxoSmithkline ambao ndio waliokuwa
wazungumzaji wakuu.
Na Mwandishi Maalum
Tatizo
la wanafunzi wa kike kutochangamkia au kuyapenda masomo ya sayansi,
teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) ni tatizo linalozikumba
nchini nyingi duniani zikiwamo zilizoendelea.
Na
kwa sababu hiyo imeelezwa kwamba, ushirikiano wa karibu kati ya
serikali kuu, sekta binafsi, wazazi , walimu na wanafunzi wa kike
unahitajika hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote na hasa wakati
huu ambapo Jumuiya ya kimataifa inajipanga na kuandaa ajenda mpya za
malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2015.
Hayo
yamejitokeza siku ya jumatano wakati wa mkutano wa pembezoni
ulioandaliwa kwa pamoja kati ya Tanzania, Uingereza na Kampuni ya
Kimataifa ya GlaxoSmithkline na kuwashirikisha wajumbe wanaohudhuria
mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake unaoendelea hapa
Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Katibu
Mkuu, kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Jinsai, Bibi
Anna Maembe kwa upande wa Tanzania, Bibi Maria Miller ( Mb) Waziri wa
Wanawake na Usawa kwa upande na Uingereza na Bibi. Nicola Yates Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Madawa ya Uingereza na Ireland na
Meneja Mkuu wa GlaxoSmithkline ndio waliokuwa wazungumzaji wakuu wa
mkutano huo ambao dhumuni lake lilikuwa ni kutafakari, kubadilisna
uzoefu, changamoto na kutafuta mbinu zaidi za kuwasaidia wanafunzi wa
kike kupenda STEM.
Mkutano
huo ambao ulivutia washiriki wengi hadi wengine kukosa nafasi ya
kuingia, modereta wake alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bibi.
Irina Bokova.
Akielezea
uzoefu wa Tanzania na changamoto zake katika eneo hilo , Katibu Mkuu
Anna Maembe, amesema, pamoja na kwamba serikali kuu kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali zikiwamo sekta binafsi kuweka mifumo mbalimbali
inayolenga kuwasaidia na kuwahamasisha watoto wa kike kuchangamkia
masomo hayo bado safari ni ndefu.
Akasema
changamoto kubwa ni katika eneo la ufuatiliaji ili kubaini kama
wanafunzi waliosaidiwa na kujengewa uwezo wamefikia wapi katika masomo
yao na baada ya kuhitimu je wanafanya kile walichosomea.
Akaongeza
kuwa itakuwa ni kazi bure kama serikali peke yake itaachiwa jukumu
hilo pasipo wazizi wenyewe kuhamasika na kuwajengea mazingira mazuri
watoto wao wakike tangu wakiwa na umri mdogo wa kuyapenda masomo hayo.
“Sisi
katika Tanzania tunaishukuru sana serikali kwa mchango wake wa
kuwasaidia wanafunzi wa kike kujiunga na masomo ya sayansi, hesabu,
uhandisi na teknolojia, lakini serikali peke yake haiwezi kufanya kila
kitu, nafasi ya wazazi ni muhimu sana sana” akasisitiza.
Akaongeza
pia kuwa Tanzania inao wanawake ambao ni wahandisi, wataalamu
waliobobea katika ufundishaji wa hesabu, sayansi na hata utafiti na
wengine wanaongoza Idara za Serikali au kampuni binafasi.
Akasema hao wote wanaowajibu wa kujitokeza ili kutumia uzoefu wao kuwahamasisha wanafunzi wa kike kufikia pale walipofika wao.
Naye
Waziri wa Uingereza yeye alisema, hata katika nchi yake, bado
wanafunzi wengi wa kike hawapendi masomo hayo, na hata kama wakiyasoma,
si wote waoishia kufanya kazi walizosomea.
Akasisitiza
haja na umuhimu wa sekta binafsi kusaidiana na serikali katika eneo
hilo na pia umuhimu wa watoto wa kike kuhamasishwa na kujengewa uwezo
wakiwa wangali wadogo ili kutambua vipaji vyao.
Naye
Makamu Rais na Meneja Mkuu wa GlaxoSmithKline yeye aliainisha
program mbalimbali ambazo kama sekta binafsi imekuwa ikichangi katika
eneo hilo.
Akasema
uzoefu uonyesha kuwa watoto wa kike wakiwezeshwa na kuhamasishwa
wakiwa wangali wadogo wanayofursa kubwa ya kupenda hesabu, sayansi,
uhandisi na masuala ya teknolojia. Na pia inakuwa hamasa kwao wakiwaona
wanawake waliofanikiwa katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment