EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, April 25, 2014

Hii hapa top 20 ya 'Mama Shujaa wa Chakula' watakaoingia kijiji cha Maisha Plus wikiendi hii

Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na kusimamiwa na Oxfam limefikia tamati ya hatua ya awali ya kutafuta washindi kwa kutangaza wanawake 20 kuingia katika top 20 ya shindano hilo la aina yake.

Wanawake hao wenye wasifu tofauti tofauti sasa wataingia katika kijiji cha maisha plus kwa muda wa wiki tatu ikiwa ni katika hatua ya kutafuta mshindi wa shindano hilo ambalo linalenga kuhamasisha jamii juu ya kilimo, hifadhi ya chakula na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na njaa. Mbali na wanawake hao 20 pia kuna mshiriki mmoja ambaye yeye amepatikana kwa shindano la mtandaoni.

Hapa nakuletea orodha ya akina mama hao mmoja baada ya mwingine. 

GRACE G.D MAHUMBUKA (46) mkazi wa Karagwe Kagera nambari yake ya ushiriki ni MS 08, ni mkulima wa shamba la ekari 18 na na mfugaji wa ng’ombe, kondoo na mbuzi.


ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anawahamasisha wana kijiji kutumia vyema mvua za kwanza na kupanda miti kwa ajili ya utunzaji wa vyanzo vya maji na kutunza mazingira."Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 18. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 35"


NEEMA URASSA KIVUGO (48) (Mshindi: Mama Shujaa wa Chakula Mtandaoni) ni mkazi wa Kiteto Manyara, namba yake ya ushiriki ni MS 12, na mkulima wa shamba la ukubwa wa ekari 10. 

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Yeye ni mchapakazi na anachukulia kilimo kama njia ya kumkwamua dhidi ya umasikini. Yeye ni mbunifu na hujifunza kwa haraka. Anavuna mazao gunia 78 kwa mwaka.


MARY JOHN MWANGA (52) ni mkazi wa Mkalama Singida, ni mkulima na mfugaji anashamba la ekari 5 na analima mahindi na anafuga ng’ombe watano

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anashiriki katika shughuli za maaendeleo ya kijiji, michango na mikutano. "Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 22" anasema.


DORICUS MSAFIRI SHUMBI (38) namba yake ya ushiriki ni MS 25 ni mkazi wa Mkalama Singida, mkulima na mfugaji, ana shamba la ukubwa wa ekari 5 ambayo anaitumia kulima mahindi, anafuga ng’ombe 5.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anapenda kujitoa na kushirikiana na vikundi mbalimbali "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 7. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 56" anasema

KURUTHUMU RAMADHANI MWENGELE (48) namba yake ya ushiriki ni MS27, ni mkazi wa Korogwe Tanga na ni mkulima na mfugaji analima ekari 6 na anafuga kuku 6, mbuzi 6 na bata 4.



ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anashirikiana na wenzakekupeana mawazo kwa ajili ya ufugaji bora na kilimo cha kisasa. "Kwa mwaka ninavuna hoho 8,000 na tango 7,000" anasema


MARY ATHANAZ NDASI (38) mkazi wa Sumbawanga Rukwa namba yake ya ushiriki ni MS 21 yeye ni mfugaji wa kuku.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu kutokana na mradi huu ameweza kujenga na kulipa karo za shule za watoto na familia inapata chakula cha kutosha. Anasema "Kwa mwaka ninapata trei 4,320 za mayai"


SANTINA MAPILE (27) mkazi wa Njombe namba yake ya ushiriki ni MS 20 ni mfugaji na anafuga nguruwe.



ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu amewahi kupata mafunzo ya ujasiriamali na akabahatika kupata mkopo na kurejesha kwa wakati. Anasema "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 1.5. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 15"


THEREZA KITINGA (44) mkazi wa Sengerema Mwanza namba yake ya ushiriki ni MS 18, ni mkulima wa shamba la ukubwa wa ekari 10.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anazingati ataratibu za kilimo cha kisasa na anshirikiana na wenzie kuzalisha mazao mengi ili kujihakikishia chakula kingi. "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 10. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 80"


NEEMA GILBERT UHAGILE (28) mkazi wa Njombe namba yake ya ushiriki ni MS 19 ni mkulima na mfugaji ana ekari 2 anazolima mahindi, maharagwe na maparachichi na anafuga kuku na ng’ombe.



ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anapenda kazi ya kilimo  na ufugaji na pia anajiamini katika kazi yake. Anasema "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 2. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 10 na ninapata mayai trei 200"


FREDINA M SAID (43) mkazi wa Kishapu Shinyanga namba yake ya ushiriki ni MS 22 ni mkulima na ana sahamba lenye ukubwa wa ekari 12.



ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anabuni njia mbalimbali za kumuingizia kipato na pia anaunda vikundi vya kijasiriamali na anaendesha mdahalo kwa wanawake ili wajitambue. "Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 67" anasema


ESTHER KULWA (57) mkazi wa Simiyu namba yake ya ushiriki ni M 23 ni mfugaji na mkulima na ana shamba la ukubwa wa ekari 7 anazotumia kulima mpunga na mahindi, pia anafuga ng’ombe 7.



ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababuanahamasisha akina mama kuwa wajasiriamali kupitia kilimo na kupata mitaji. "Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 90" anasema


JOYCE NORMANI HASSAN (44) mkazi wa Masasi Mtwara nambari yake ya ushiriki ni MS 16 ni mkulima na ana ekari 2 za mahindi, korosho na mbogamboga.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anaendesha kilimo cha kitaalamu na pia amejiunga na vikundi mbali mbali. "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 6. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 27"


ELIZABETH SIMON mkazi wa Kilosa Morogoro namba yake ya ushiriki ni MS 15 ni mkulima wa mahindi na mpunga ekari 2 na mfugaji wa ng’ombe, mbuzi na kondoo.



ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anajishughulisha na kilimo. "Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 20 na ninapata lita 5,000 za maziwa"


ZINAIDA JAMES KIJERI (40) mkazi wa Kakonko Kigoma, namba yake ya ushiriki ni MS 10, ni mkulima wa shamba la ukubwa wa ekari 7 na mfugaji wa ng’ombe 10 na mbuzi 15.


ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anajiamini na anajituma katika shughuli mbalimbali na pia kushauriana na wafugaji wengine pamoja na wakulima. Anasema "Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 30 na ninapata lita 1,825 za maziwa"


ELINURU MOSES PALLANGYO (52) mkazi wa Meru Arusha, namba yake ya ushiriki ni MS 01, ni mkulima na mfugaji ana shamba la ukubwa wa robo tatu ekari, analima ndizi na mboga na kufuga ng’ombe, mbuzi na kuku.



ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Anajituma na kazi yake inaonekana, watu kutoka ndani na nje ya nchi, vikundi, mashirika naa watu binafsi huwenda kujifunza katika darasa lake la kujitolea. Anasema "kwa mwaka ninavuna ndizi mikungu 70, ninapata kilo 336 za nyama za kuku pamoja na maziwa lita 3780"


LEAH DOMINICK MNYAMBUGWE (52) mkazi wa Dodoma Mjini namba yake ya ushiriki ni MS 03, yeye ni mkulima na mfugaji ana shamba la ukubwa wa ekari 21.


ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu mifugo insaidia kupata kipato pia kuelimishana kuhusu ufugaji wa kisasa na kupata mazao bora. "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 21. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 40 na ninapata lita 1,460 za maziwa"


DOROTHY DANIEL PALLANGYO (64) mkazi wa Meru Arusha, namba yake ya ushiriki ni MS 02 yeye ni mkulima na mfugaji ana shamba la ukubwa wa ekari 2 na anafuga ng’ombe na mbuzi.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA:  Kwa sababu Anafuga kisasa na ana banda bora la mifugo, pia analima kwa kuotesha kwa kufuata ushauri wa kitaalamu. "nina shamba lenye ukubwa wa ekari 2. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 30 na ninapata lita 5,040 za maziwa"
UPENDO MBAZI MSUYA  (38) ni mkazi wa Mwanga Kilimanjaro nambari yake ya ushiriki ni MS 11, ni mkulima wa shamba lenye ukubwa wa ekari 2 na mfugaji wa ng'ombe 3.


ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu mara nyingi huwashauri wakulima wenzie kulima kwa wakati na kupanda mbegu bora na kwa kipimo, kutumia mbolea na kunyunyizia dawa pindi wadudu wanapoharibu mazao. "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 2. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 20"

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate