EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, April 11, 2014

KINANA AMALIZA KWA KISHINDO ZIARA YAKE WILAYANI BUHIGWE LEO, AKAGUA MIPAKA YA TANZANIA NA BURUNDI KWENYE WILAYA HIYOKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni mpaka kati ya Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma leo Alhamisi, Aprili 10, 2014. Kinana yupo katika ziara ya siku tano mkoani humo ya kukagua uhai wa Chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani humo. Moja ya kero kwenye mpaka huo unaokutanisha vijiji vya Kibande (Tanzania) na Murambi(Burundi) ni Watanzania kulazimika kukumbana na adha ya kuvuka mto huo kwenda kufanya biashara na kununua mahitaji kwenye soko lililopo upande wa Burundi. Wa pili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
Kinana akitazama mpaka huo na namna wananchi walivyokuwa wakivuka na wengine kuvushwa kwenye mto wa Malagarasi wakitoka Burundi kuingia Tanzania
 Eneo la soko la Murambi, Burundi ambako Watanzania hulazimika kwenda kufanyabiashara na kupata mahitaji huko kutokana na upande wa nchi yao kutokuwa na soko ikiwemo la mifugo lililokuwepo zamani na sasa halipo kutokana na kufungwa kwa sababu zisizojulikana, ambaopo Kinana alihoji kwa nini lisiwepo soko upande wa Tanzania ili kuondoa kero ya watu kuvuka mto kila siku kwenda ng'ambo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa pembezoni mwa mto Malagarasi, mpakani mwa Tanzania na Burundi wakati wa ziara hiyo.
 
 
 Juu ya maelezo haya ni wananchi wakivuka mto Malagarasi kutoka upande wa Burundi kuingia Tanzania
Baadhi ya wananchi wa Burundi wakiwa wameingia Tanzania baada ya kuvuka mto huo kwa taabu, baadhi yao wameomba serikali za nchi hizo kujenga daraja kwenye mto huo kurahisisha uvukaji
 Wananchi wa Kijiji cha Buhigwe wakimlaki Kinana alipowasili kwenye Ofisi ya CCM Kata ya Buhigwe, kuzungumza na Kamati ya Siasa ya CCM wilayani humo, leo
Kinana akizungumza na wananchi hao baada ya kumaliza kuzungumza na Kamati hiyo ya siasa. Kulia ni Mbunge wa Buhingwe maarufu kwa jina la Obama
'Obama' akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa michezo Kata ya Buhigwe.
Mwakilishi kutoka Burundi akitoa salam za wananchi wa mpakani, kwenye mkutano huo wa Buhigwe
 Katibu Mkuu wa CCm Abdulrahman Kinana akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Buhigwe wakati wa mkutano huo
Katibu wa NEC, Itkadi na Uenezi, Nape Nnauye akicharaza ngoma na kikundi cha Kerebuka kilipotumbuiza kwenye mkutano wa Kinana na wananchi wa Buhigwe

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate