WABUNGE wa Bunge Maalum la Katiba wanaokutana mjini Dodoma kujadili
namna ya kupata Katiba Mpya wamekuwa wakijinasibu kuwa, wanawawakilisha
wananchi wa Tanzania katika kupata katiba iliyo bora.
Unaweza kuwepo uongo, lakini huu wa kuwasingizia Watanzania kuhusu kupatikana kwa Katiba Mpya ni uongo mkubwa ambao sijui wanaouanzisha wana malengo gani na taifa hili? Nikiulizwa kwa nini? Nitasema kwa kiapo kuwa, hakuna Mtanzania halisi aliyewahi kuwa na haja ya kupatikana kwa Katiba Mpya!
Mwenye kunihoji kuhusu Watanzania halisi ninaowazungumzia, nitamwelewesha kuwa ni wale waishio vijijini na waliopo mjini ambao wamekosa fursa ya kupata elimu bora ya kuwawezesha kujitambua.
Mwananchi halisi ninayemzungumzia hawezi kuwa Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, si Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wala Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ni Mwanamangwengwe wa Itaga mkoani Tabora ambaye hajui kusoma wala kuandika sambamba na familia yake yote.
Anayekubaliana nami katika hili aitike: ‘Amini’, kwa kuwa nchi hii wananchi wake walio wengi ni wale wa kutoka katika kundi la Mwanamangwengwe wala si la akina Kinana. Kama ni sahihi, anayesema anawawakilisha wananchi lazima awe amepata kibali kutoka kwa wapwa zangu wa Ujiji mkoani Kigoma na si wakazi wa Msasani kwa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Najiuliza,“ni lini wanasiasa wametumwa kutafuta Katiba Mpya badala ya kuwaletea wananchi maendeleo?” Swali la nyongeza anawezaje mtu kukutuma kitu kipya wakati hata kile cha zamani hakifahamu?
Acheni kucheza na akili za watu ninyi binadamu! Haiwezekani mkutane Dodoma na kauli mbiu ya kuwatungia Watanzania Katiba Mpya wakati ile ya zamani mliwanyima fursa ya kuitambua na kiukweli wananchi walio wengi hawaifahamu kabisa.
Ikiwa ni hivyo, katiba ya zamani imewakera nini mpaka watake mpya? Ukisikiliza vimbwanga vya ‘wanjanja wa kisiasa’ utasikia wakisema: “tumewahoji wananchi kadhaa na wengi kati yao wametaka Muundo wa Serikali Tatu,
” hivi wananchi kutaka Muundo wa Serikali Tatu au Mbili ndiyo kutaka Katiba Mpya? Utoto kabisa huu! Kwa kuwa kila Mwanasiasa ameshatambua udhaifu wa wananchi, basi kila mmoja vazi lake ni kutumwa na wananchi.
Kila siku vinaibuka vikundi na mangenge ya kila aina yanayoundwa ndani na nje ya bunge yakijifanya kutafuta katiba ya wananchi, aliyewatuma ni nani? Nashauri, kama wanasiasa wameshindwa kuwafanya
Watanzania kuwa na maisha bora na umoja wa kitaifa ni heri wasichume majanga ambayo naamini hawatayala na familia zao. Tuachane na ujanja wa senene. Nachochea bunge la katiba ni la wanasiasa si la wananchi!

No comments:
Post a Comment