Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Palycarp Kardinali Pengo amekema ndoa za jinsi moja na zile za mkataba kwa sababu ni kinyume cha maadili ya dini zote na zinachangia kuharibu familia.

Akizungumza katika sikukuu ya mapadri na kubariki mafuta ya krisma katika Kanisa la Mtakatifu. Joseph, Dar es Salaam, Pengo alisema ndoa za mkataba zinachangia kwa kiasi kikubwa wanandoa kutokuwa waaminifu na kujiingiza katika vitendo viovu ambavyo vinazaa familia ambazo hazina maadili.Kuna wanandoa wanaona kukaa na mwenza wake kwa muda wote ni jambo ambalo halikubaliki, wanajiingiza katika ndoa za mkataba ili waweze kufanya matendo mengine ambayo hayampendezi Mungu na hapo ndipo wanajenga familia isiyokuwa na maadili,¡± alisema.

Kuhusu ushoga, Pengo alisema: ¡°Hatuwezi kuwa na familia imara kama hatutakemea mazingira haya ya ndoa za jinsi moja na hatuwezi kuzungumzia uhai wa kuwa na familia bora wakati kuna kikwazo ambacho hakiendani na maadili ya dini zote.¡

Kardinali Pengo pia aliwaonya mapadri wanaotumia fedha za kanisa kwa masilahi binafsi akiwataka kuacha tabia hiyo mara moja. Alionya kwamba endapo watabainika, kanisa halitatoa fedha kulipa faini au fidia itakayotokana na uzembe huo.

Aliwashukuru waumini wa Dar es Salaam kwa kumpatia zawadi ya Sh43 milioni wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya uaskofu na kuahidi kuzitumia katika ujenzi wa Shule ya Msingi Kisiwani iliyopo Mafia.

MCL