Na Joseph Shaluwa na Musa Mateja
MARADHI yanayomsumbua mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ni tishio, Gazeti la Mastaa, Amani limeelezwa.
Ray C anaugua ugonjwa wa Homa ya Dengu ambao kitaalam hujulikana kama
Dangue Fever. Ulibainika baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa
Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni, Mwananyamala jijini Dar na
baadaye kulazwa hospitalini hapo.
Staa huyo wa muziki ambaye pia hujulikana kama Kiuno Bila Mfupa
alifikishwa hospitalini hapo, Jumapili iliyopita mchana baada ya hali
yake kuwa mbaya.
KUTOKA KWA CHANZO
“Ni kweli Ray C amelazwa hapa
Mwananyamala. Ameletwa leo (Jumapili) saa tano mchana,” alisema mtoa
habari wetu ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.
Mtoa habari huyo, naye alikuwa mgonjwa alilazwa katika wodi namba tano, hospitalini hapo ambayo Ray C alikuwa amelazwa.
“Afya yangu si nzuri sana, lakini nimeweza kumtambua. Namfahamu sana
Ray C. Nina hakika ndiye aliyelazwa hapa,” aliendelea kusema lakini
hakueleza ugonjwa anaougua.
MAPAPARAZI WAINGIA KAZINI
Baada ya timu yetu
kunasa taarifa hizo, Jumatatu jioni mapaparazi wetu walitinga
hospitalini hapo na kuthibitishiwa kuwa Ray C alikuwa mgonjwa na
kulazwa.
Hata hivyo, juhudi za kuingia wodini kuonana naye hazikuzaa matunda
kwa vile muda wa kuwaona wagonjwa ulikuwa umekwisha kwa siku hiyo.
Hata pale walipojitambulisha kuwa ni waandishi, wahusika walijibu kwa kifupi: “Haiwezekani, anatakiwa kupumzika.”
DAKTARI ATHIBITISHA
Mmoja wa madaktari
wanaoshughulikia afya ya msanii huyo alithibitisha kuwa Ray C ana dalili
zote za ugonjwa huo, akasema: “Ni kweli ana dalili zote za dengu,
lakini siruhusiwi kutoa taarifa za mgonjwa, labda kwa ruhusa yake
mwenyewe au mama yake mzazi.”
AMANI TENA
Waandishi wetu hawakuchoka, siku
iliyofuata, Jumanne asubuhi na mapema, mapaparazi walidamkia hospitalini
hapo kwa lengo la kumjulia hali staa huyo lakini walipoingia wodi namba
tano alipokuwa amelazwa, hakuwepo!
Ilikuwa ni muda wa kuwaona wagonjwa, waandishi wakakuta kitanda
kitupu, walipouliza kulikoni wakaelezwa amehamishiwa wodi maalum.
“Amehamishiwa
kwenye chumba maalum kwa sababu waandishi walikuwa wanasumbua sana
kutaka kumuona. Kama unavyojua tena, wodi ya kawaida inakuwa haina
uangalizi mkubwa.
“Mtu yeyote anaweza kuingia ikiwa tu muda wa kuwaona wagonjwa utakuwa
umefika. Jambo hilo limewakera sana ndugu ndiyo maana wamezungumza na
madaktari na kumhamisha,” mtoa habari mwingine alisema kwa sharti la
kutotajwa jina lake gazetini.
UFAFANUZI
Daktari mwingine aliyezungumza na
Amani hospitalini hapo kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini kwa
vile si msemaji alisema: “Kuhusu kulazwa, ni kweli amelazwa na anaumwa,
lakini kumuona ni ngumu.
“Unajua Ray C ni maarufu, kumuacha kwenye wodi ya kawaida ni
kumsababishia usumbufu usio na maana, wengi wanataka kumuona hasa
waandishi kama ninyi. Anahitaji kupata muda wa kutosha kupumzika.”
KWA NINI TISHIO?
Homa ya Denge (Dengue Fever)
kama ilivyoelezwa hapo juu ni tishio. Virusi vya ugonjwa huu husabazwa
na mbu aina ya Aedes ambaye yupo katika mgawanyiko wa jamii tisa; Aedes
Australis, Aedes Albooictus, Aedes Aegypti, Aedes Contator, Aedes
Cinereus, Aedes Ructcus, Aedes Polynesiensis, Aedes Scutellaris na Aedes
Vexans.
Mbu wa kike aina ya Aedes anapomng’ata binadamu mwenye maambukizi ya
Homa ya Dengu huanza kuathirika mwenyewe na baada ya siku 8-10
huathirika zaidi kiasi cha mate yake kubeba virusi vya homa hiyo.
Dengu pia husambazwa kwa njia ya kuongezewa damu au kupewa viungo vya
mtu aliyeathirika. Inawezekana kwa mama kumwambukiza mtoto wakati wa
ujauzito au kwenye kujifungua.
Yapo maambukizi ya mtu na mtu wakati
wa kujamiiana au mwingiliano wa damu lakini kitaalam inafafanuliwa
kwamba si kawaida hali hiyo kutokea.
Ugonjwa huo unadhibitiwa kwa kumpa mgonjwa dawa ili kuzuia kutapika,
maumivu ya mwili na kupewa dripu za maji lakini hakuna dawa maalum za
tatizo hilo na mgonjwa akipona huweza kuugua tena siku yoyote.
TAARIFA ZAIDI ZA KIDAKTARI
Gazeti hili liliwahi
kufunga safari hadi Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni, Dar na
kufanikiwa kuzungumza na mganga mkuu wa hospitali hiyo ambaye hakutaka
jina lake liandikwe gazetini.
Alithibitisha kuwepo kwa gonjwa hilo baya ambapo wakazi wengi wa jiji wameugua na wapo wanaoendelea kuugua.
“Huu ugonjwa haujaanza leo, inaonekana kama hospitali hii inahusika
kwa kiasi kikubwa na tatizo hilo kwa sababu mimi niliamua kuachana na
habari za kuwatibu watu malaria tu nikawa makini kutazama na ugonjwa huu
ambao wengi hawautilii mkazo,”alisema.
Daktari huyo alizidi kusema kuwa, ugonjwa huo unaenezwa na mbu weusi
wanaorandaranda ambao wanapenda kukaa sehemu zenye uchafu na majimaji.
“Wale mbu weusi wanaeneza kwa kasi ugonjwa huu ni tofauti kabisa na wale wanaoneza ugonjwa wa malaria,” alisema.
Akielezea dalili za ugonjwa huo mganga huyo alisema zinafanana na
zile za ugonjwa wa malaria, mtu kuhisi joto kali mwilini, maumivu ya
kichwa, kutapika, tumbo, maumivu ya mwili na misuli.
Alisema ugonjwa huo ulizidi kushika kasi mwaka huu katika kipindi cha
mafuriko hivyo idadi ya wagonjwa aliowatibu kwenye hospitali yake
ikaongezea, kutoka wagonjwa 4 mwaka jana mpaka kufikia wagonjwa 20 tangu
Januari, 2014 kutokana na mvua iliyosababisha kuwepo kwa madimbwi kila
kona.
MPAKA SASA HAUNA TIBA
Ugonjwa huu mpaka sasa
hauna tiba ya uhakika, kinachifanywa kwa wagonjwa wanaogudulika kuwa nao
ni kutibiwa tu dalili ili usizidi kusambaa mwilini.
WALIOATHIRIKA
Taarifa kutoka kwa wataalamu wa
afya zinasema kuwa, mpaka sasa takribani watu milioni 100 duniani kote
wameambukizwa ugonjwa huo na wengine milioni 2 wamefariki dunia baada ya
kuugua.
TUMUOMBEE
Hata hivyo, jambo muhimu kwa
Watanzania wote na wapenda burudani ni kumuombea Ray C apate nafuu
haraka na kurejea kwenye majukumu yake kama kawaida.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Ray C kwa muda mrefu alikuwa
na matatizo ya kiafya lakini hivi karibuni afya yake ilitengemaa na
usiku wa Jumamosi ya Mei 3, mwaka huu (kuamkia siku aliyolazwa)
alionekana akiwa mwenye afya njema katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar
kwenye shughuli za tuzo za muziki za Kilimanjaro Tanzania Music Awads
(KTMA).
Ilikuwa mara ya kwanza kwa msanii huyo kuonekana hadharani baada ya
kujificha kwa muda mrefu kufuatia matatizo yake ya kuugua kutokana na
matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’.
GLOBAL ILISHAANDIKA KUHUSU DENGU
Kuibuka kwa
ugonjwa wa Homa ya Dengu kuliripotiwa kwa mara ya kwanza kwenye gazeti
la Risasi Jumamosi ya Mei 3,2014 likiwa na kichwa cha habari ukurasa wa
mbele kisemacho:GONJWA LISILO NA TIBA YA UHAKIKA LAIBUKA.
Ray C aliruhusiwa kutoka hospitali juzi saa 9:50 baada ya afya yake kuimarika.
Thursday, May 8, 2014
GONJWA LA RAY C HATARI, LAPUKUTISHA WATU MIL 2, MIL 100 WAAMBUKIZWA!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment