Mohammed Mdose na Said Ally
MAMBO yanazidi kuwa mambo kwenye usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara! Wakati Azam FC ikiwa imejihakikishia kumtumia kiungo mkabaji, Frank Domayo kuanzia msimu wa 2014-2015, tamko zito limetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya usajili huo.
TFF imetoa tamko kuwa mpaka sasa bado haiutambua usajili wa kiungo
huyo kutoka Yanga kwenda Azam FC, ikiwa na maana kuwa kwa TFF husajili
huo haupo.MAMBO yanazidi kuwa mambo kwenye usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara! Wakati Azam FC ikiwa imejihakikishia kumtumia kiungo mkabaji, Frank Domayo kuanzia msimu wa 2014-2015, tamko zito limetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya usajili huo.
Shirikisho hilo limesema kuwa usajili huo kutambulika au kutotambulika itajulikana mara baada ya majibu ya ripoti ya uchunguzi wa usajili huo itakapopitiwa na kutolewa ufafanuzi, ambapo mpaka sasa ipo mezani kwao ikiwa imekamilika.
Ufafanuzi huo umetolewa na Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine ambaye amesema kuwa TFF haijapitisha wala kutambua usajili huo kwa kuwa ulikuwa ukisubiri ripoti ya uchunguzi wa Domayo ambaye inadaiwa alisajiliwa na Azam wakati akiwa kambini kwenye timu ya taifa, Taifa Stars, Tukuyu mkoani Mbeya, wiki kadhaa zilizopita.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwesigwa alisema uchunguzi zaidi ulikuwa ukifanyika kama ilivyoagizwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, lakini akasisitiza kuwa tayari umeshakamilika na kilichobakia ni kupitiwa kisha kutolewa maamuzi kama Azam walikiuka kanuni au walikuwa sahihi kwa huo mchakato wao wa kutaka kumsajili Domayo akiwa ndani ya majukumu ya Stars.
“Suala la Domayo ni jambo kubwa na la kisheria, hivyo hatuwezi kulichukulia kirahisi, tulitoa muda wa siku 14 kufanyika kwa uchunguzi kwa ajili ya mwanasheria wetu kulifanyia kazi.
“Kwa sasa hatuwezi kulizungumzia mpaka pale ripoti itakapotolewa, kwani tayari ameshaikamilika na ameiwasilisha, kilichobaki ni kupitiwa na kutolewa maamuzi sahihi juu ya kilichotokea siku husika,” alisema Mwesigwa.
No comments:
Post a Comment