KUTOKANA na tukio lililotokea jana Aprili 30 mwaka
huu kwenye kambi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) iliyopo Tukuyu mkoani
Mbeya likihusisha usajili wa baadhi ya timu, Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza
mlolongo mzima wa tukio hilo.
Taarifa ya TFF imesema kwamba, baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua.
TFF imesema katika taarifa yake inatoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao.
Viongozi wa Azam FC jana walikwenda kwenye kambi ya Taifa Stars kukamilisha taratibu za usajili na kiungo Frank Domayo, aliyemaliza Mkataba wake Yanga SC.
Baada ya kufanikiwa kumsainisha Mkataba wa miaka miwili, wasimamizi wa kambi waliwaitia Polisi viongozi wa Azam FC ambao hata hivyo baadaye waliachiwa.
Lakini inadaiwa fomu za usajili zilichanwa.
CHANZO: BIN ZUBEIRY

No comments:
Post a Comment