EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, May 1, 2014

BAJETI KUU YA SERIKALI: TAKRIBANI SH. TRIL. 19. 7 ZATARAJIWA KUTUMIKA MWAKA 2014/2015


Spika wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwaasa wabunge wote kushiriki kikamilifu katika kamati zao kizalendo kwa kujali nchi yao ili ipatikane bajeti yenye tija kwa taifa leo (jana) wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya  Salum akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti kuu ya Serikali kwa wabunge leo (jana)  jijini Dar es salaam inayotarajia kuanza kutumika kwa mwaka wa fedha unaoanza Julai 2014/2015.
Waziri Mkuu wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda  akizungumza na wabunge wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha Saada Mkuya akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt.Mary Nagu kabla ya kupokea taarifa ya bajeti ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam.  
BAJETI KUU YA SERIKALI: takribani Sh. Tril. 19. 7 zatarajiwa kutumika mwaka 2014/2015
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali imepanga kutumia jumla ya sh.19, 653.31 ambayo ndiyo sura ya bajeti katika mwaka wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo ya nchi na watu wake.
 Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipokuwa akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti kuu ya Serikali inayotarajia kuanza kutumika mwaka wa fedha unaoanza Julai 2014/2015 leo (jana) jijini Dar es salaam.
Waziri Saada alisema kuwa mfumo wa bajeti kwa mwaka wa fedha unaoanza unazingatia sera za bajeti kwa mwaka 2014/2015 ambazo zitazingatia vipaumbele vya mpango wa Maendeleo wa Taifa  na malengo ya utekelezaji wa mkakati wa matokeo makubwa sasa (BRN).
 Kwa upande wa matumizi ya kawaida Serikali inatrajia kutumia jumla ya sh.trilioni 14, 208. 21 ambayo inajumuisha mfuko mkuu wa serikali, mishahara ya watumishi wa Serikali, wizara, mikoa, halmashauri, taasisi na wakala za Serikali.
Aidha, kwa matumizi mengine yatakuwa ni kwa ajili ya maendeleo kwa mwaka wa fedha unaotarrajiwa kuanza Julai mwaka huu ambapo kiasi cha 5, 445.10 ambazo ni sawa na asilimia 27.7 zimepangwa kutumika kwa kuhusisha fedha za ndani na za nje ya nchi.
Waziri Saada akiwasilisha taarifa yake kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge hao waliipokea Taarifa ya Serikali kuhusu Makadirio ya Bajeti katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam ambayo inatarajiwa kuongeza wigo wa wabunge kuijadili bajeti hiyo kabla ya kusomwa bungeni mjini Dodoma.
Shabaha ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha ni kuhakikisha pato la taifa litakuwa kwa asilimia 7.2 mwaka 2014, asilimia 7.4 mwaka 2015, asilimia 7.7 mwaka 2016 na kuendelea kuongezeka hadi kufikia asilimias 8.0 ifikapo mwaka 2017.
Misingi ya bajeti ya Serikali kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 ni pamoja na kuendelea kuwepo na kuimarishwa amani, usalama, utulivu na utengamano misingi ambayo itasaidia kupatikana kwa katiba mpya kwa wakati kama ilivyopangwa.
Kwa upande wake Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira akiwasilisha rasimu ya mpango wa maendeleo wa taifa katika bunge likikaa kama kamati alisema kuwa maeneo ya  vipaumbele yanalenga miradi ya kitaifa ya kimkakati inayolenga kutanzua vikwazo vikuu vya kiuchumi inajumuisha miundombinu ya uasfirishaji kama reli, barabara, bandari, na usafiri wa anga.
Vipaumbele vingine ni nishati, huduma ya maji mijini na vijijini, kilimo, viwanda, maendeleo ya rasilimali watu na huduma za kiuchumi kama fedha, biashsra na utalii.
Naye Spika wa Bunge  la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amewaasa wabunge wote washiriki kikamilifu katika kamati pamoja na serikali ili ipatikane bajeti yenye tija kwa taifa na wabunge waikamilishe kizalendo kwa kujali nchi yao.

Kikao cha Bunge la bajeti kinatanguliwa na kamati mbalimbali zitakutana ambapo vikao vilianza Aprili 27, 2014 kwa wajumbe kuwasili jijini Dar es salaam na kuhitimishwa Mei 4, 2014 na wabunge kuanza safari kwenda Dodoma tayari kwa kuanza kikao chake kama ilivyopangwa.

Kamati ya bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakati wa Bunge la bajeti, kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, kamati ya Nishati na Madini, kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) kujadili hesabu zilizokaguliwa za Serikali kuu na mashirika ya umma, kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa.

Na nyingine ni kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,  kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,  Sheria na Utawala, kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara,  kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI, kamati ya LAAC Dar es salaam na kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamii.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate