EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, May 9, 2014

WEMA ANASA USHAHIDI KAJALA KUMUIBIA BWANA


Stori: IMELDA MTEMA
Unaweza ukaficha siri na ukaamini hakuna atakayejua bila kukumbuka kuwa hakuna siri ya watu wawili! Hatimaye Wema Isaac Sepetu amenasa ushahidi wa aliyekuwa rafikiye kipenzi, Kajala Masanja wa kumwibia aliyekuwa bwana’ke, Clement au CK, yule kigogo wa ikulu.
Wema Sepetu.
MIL. 13 KISINGIZIO TU
Habari za mjini kwa wiki nzima ni kusambaa kwa ujumbe mfupi (SMS) za kimapenzi za Kajala na CK ambazo sasa zimefunua kisa kamili cha mastaa hao kuhitilafiana huku Sh. Milioni 13 zikiwa kisingizio tu.
WEMA ALIKUWA ANATAFUTA USHAHIDI?
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na mastaa hao, kupatikana kwa meseji hizo ni kama mpango wa Mungu, kwani sasa kitendawili kimeteguka.
 
Baadhi ya meseji zilizonaswa.
“Wema alikuwa anatafuta ushahidi kama kweli Kajala anatembea na CK hivyo sasa amepata ushahidi.
“Mwenye macho haambiwi tazama na kama hujui kusoma hata picha huoni? Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako!” Kilisema chanzo hicho.
Habari za ndani zilieleza kuwa meseji hizo zilikutwa kwenye simu ya CK na mwanamke mwingine ambaye naye anadaiwa kutoka na kigogo huyo, aliyetajwa kwa jina moja la Naima aliyekwenda kumbwagia ‘zigo’ Wema kwa ajili ya ushahidi.
Kajala Masanja.
Ilisemekana kwamba Naima alimuomba simu CK kwa kuwa ya kwake ilikuwa mbovu.
Habari zilizidi kudai kuwa baada ya CK kumpa mpenzi wake huyo simu yake, kumbe zile meseji alizokuwa akichati na Kajala alikuwa amesahau kuzifuta ndipo zilipobambwa.
Mpashaji wetu aliweka wazi kwamba meseji zile zilimshangaza Naima kwa kuwa yeye alikuwa ni mmoja wa watu ambao walikuwa hawaamini kabisa kama kulikuwa na ukweli wowote kuhusu tuhuma za Kajala kutembea na CK.

NAIMA ACHANGANYIKIWA
“Yaani Naima alipoziona meseji alichanganyikiwa kabisa, alikuwa kama kachomwa sindano ya ganzi kwani alikuwa ni mmoja wa watu ambao  hawaamini kabisa kama kweli Kajala anatembea na CK.
“Naima alipokaa vizuri ndipo akaanzisha timbwili lenye ujazo mkubwa na CK,” kilisema chanzo hicho.
Mnyetishaji wetu aliendelea kutiririka kuwa katika SMS hizo ambazo zilionesha waziwazi namba ya Kajala, zilikuwa zikielezea namna CK alivyokuwa akimuomba msamaha Kajala kwa kutopokea simu yake.

Kajala na Wema wakati wa ushosti wao.
HUU HAPA MZIGO
Mtiririko na meseji hizo ulikuwa hivi;
CK: “Mama mimi sipendi kukatiwa simu  pze, ok sawa lakini mi nakupenda.
Kajala: Kwa hiyo ndiyo unaniambiaje?
CK: Umeamua kuniblock?
CK: Kwa nini hupokei simu zangu?
CK: Unaponikatia simu wakati mimi naongea sijapenda sijui nijielezeje mama haya sawa.
Kajala: Fanya mambo.
MZIGO MIKONONI MWA ‘MNYAMWEZI’ WEMA
Ilisemekana kwamba baada ya Naima kuona meseji hizo alizihifadhi ili akamfikishie Wema ‘Myamwezi’ na kumuonesha jinsi rafiki yake alivyokuwa siyo mwaminfu kwake kitu ambacho alikifanikisha.
Habari zilidai kuwa baada ya Wema kuona SMS hizo alipatwa na mshtuko mkubwa kwani alikuwa haamini kama ni jambo analoweza kulifanya rafiki yake Kajala.
Ujumbe mwingine ulionaswa.
BOFYA HAPA KUMSIKIA ‘MADAM’
Baada ya ishu hiyo kuwa ndiyo habari ya mjini, gazeti hili lilijiongeza ambapo lilimsaka Wema ili kuzungumzia kuhusu meseji hizo.
Alipopatikana, Wema alifunguka kuwa  amesikitishwa mno na kitendo cha Kajala.
Wema alisema bora angefanya mtu mwingine yeyote lakini siyo Kajala aliyejitolea kuyaokoa maisha yake.
“Ukweli kabisa angefanya mtu mwingine yeyote wala isingekuwa ishu lakini siyo K. Aisee K amenishangaza na kuniumiza mno.
“Nilikuwa nimeshapanga niweke naye mambo sawa maisha yaendelee kama zamani lakini kwa hili siwezi kumsamehe tena,” alisema Wema aliyeonekana kukerwa na kucharuka vibaya.
HUYU HAPA MAMA WEMA
Baada ya kumalizana na Wema, gazeti hili lilimtafuta mama Wema, Mariam Sepetu ili kuzungumzia jambo hilo ambapo alisema kuwa siku zote alimwambia mwanaye kuwa achague marafiki wa kuwa nao lakini hakulitilia maanani.
“Unajua nilikuwa namwambia Wema kila siku, achague marafiki ambao atakuwa nao. Wengine siyo marafiki wa kweli, ndiyo kama hivyo ilivyotokea, nawaachia wenyewe mimi sina la kusema,” alisema mama Wema.
KAJALA VIPI?
Hata hivyo, gazeti lilimtafuta Kajala kwa njia mbalimbali lakini lilitonywa kuwa yupo China kwa ‘biashara zake’.
Katika mahojiano maalum na gazeti pacha la hili, Ijumaa Wikienda hivi karibuni, Kajala alikana kuwa hata na namba ya CK.
“Katika maisha yangu CK niliwahi kuonana naye mara moja tu, sina hata namba yake ya simu,” alinukuliwa Kajala.
TEAM WEMA YASHANGILIA USHINDI
Kwa upande wake lile kundi linalojiita Team Wema katika mitandao ya kijamii ilijipongeza kwa kupata ushahidi huo ambao sasa umeleta sura mpya ya ugomvi wa wawili hao.
Sehemu ya maoni mengi mitandaoni ilisomeka: “Sasa kule kulia kote runingani na mwanaye matokeo yake ndiyo haya? Kama kweli Kajala kamfanyia Wema hivyo, basi anapaswa kuomba msamaha hata kama Wema yupo na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
CHANZO NI GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate