EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, May 9, 2014

Pluijm aacha kazi Yanga

Kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van Der Pluijm.
Na Wilbert Molandi
KOCHA Mholanzi wa Yanga, Hans van Der Pluijm, ameacha kazi katika klabu hiyo.
Pluijm ameondoka nchini jana kwenda Saudi Arabia, Mashariki ya Kati barani Asia ambako ataingia mkataba wa kuinoa Klabu ya Al Shoala na atakuwa akilipwa dola 20,000 (Sh milioni 32) kwa mwezi wakati Yanga ilikuwa ikimlipa dola 11,000 (Sh milioni 18) kwa mwezi.
Pluijm alitua Yanga miezi michache iliyopita kuchukua nafasi ya Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts ambaye msimu uliopita aliipa timu hiyo ubingwa wa Bara.

Pluijm, raia wa Uholanzi, amesema amelazimika kuiacha Yanga kutokana na ofa yake kubwa aliyoipata na kilichosababisha aipate ni soka la juu walilolionyesha Yanga wakati wakiivaa Al Ahly ya Misri.
“Kweli nimepata ofa kubwa sana, lazima niondoke na nitasaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha timu hiyo. Nimewaambia Yanga na tumekubaliana, baada ya msimu mmoja nitauliza, kama watanihitaji nitarudi,” alisema.
Wakala wa Misri:
Kuhusiana na kupata nafasi hiyo, Pluijm anasema wakala kutoka nchini Misri ndiye alifanya mipango ya kumpatia timu nchini humo baada ya kuiona Yanga ikiihenyesha Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Nafikiri alianza kunifuatilia kabla, lakini baada ya mechi mbili za Al Ahly, tulianza mawasiliano naye. Mwisho akanielekeza katika ofa hiyo ya juu ambayo ninalazimika kwenda, hakuna ujanja,” alisema Pluijm ambaye aliondoka jana mchana kwa Ndege ya Shirika la Ethiopia.
Makubaliano:
Pluijm na Yanga wameingia makubaliano kwamba baada ya kusaini mkataba huo, kocha huyo arejee nchini kwa ajili ya kuwasaidia Wanajangwani.
“Bado nina mapenzi na Yanga, naona kama niko nyumbani. Hivyo nitasaini mkataba na kurudi hapa, baada ya hapo nitasafiri kwenda Ghana kusaidia kutafuta wachezaji.
“Zaidi nina mawasiliano na kiungo na mshambuliaji, ndiyo mahitaji ya Yanga. Hivyo nitatoka hapa na kwenda kufanya majadiliano kuhusiana na kuwasajili ili kukiimarisha kikosi cha Yanga,” alisema Pluijm.
Al Shaola:
Inashika nafasi ya 12 katika timu 14 zinazoshiriki Ligi Kuu Saudi Arabia na rekodi ya mechi zake tatu za mwisho inaonyesha imepoteza mbili na sare moja.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate