Staa
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. akiwa kwenye meza moja
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Ishu hiyo ilitokea mwanzoni mwa wiki baada ya kukutana jijini New
York, Marekani huku kila mmoja akiwa na majukumu yake kwenye ardhi hiyo
ya Rais Barrack Obama.
Ilisemekana kwamba JK kamkutanisha Diamond na meneja wa staa mkubwa wa muziki kutoka Marekani, Trey Songz.
Ilisemekana kwamba JK kamkutanisha Diamond na meneja wa staa mkubwa wa muziki kutoka Marekani, Trey Songz.
Kuna madai kuwa lengo la kumkutanisha Diamond na jamaa huyo ni ili
afanye kolabo na Trey Songz hivyo kumweka kimataifa zaidi kama ilivyo
kwa P-Squire.
Ilisemekana kwamba kama kolabo hiyo itafanikiwa JK atakuwa ameshiriki kuiunganisha kwa asilimia zaidi ya 90.
Ilisemekana kwamba kama kolabo hiyo itafanikiwa JK atakuwa ameshiriki kuiunganisha kwa asilimia zaidi ya 90.
Stori hiyo iliambatana na picha zilizomuonesha JK akiwa karibu na meneja wa Trey Songz huku Diamond akiwasikiliza kwa umakini.
Ilisemekana JK alizungumza na wasanii hao kwa muda mrefu katika mazungumzo ambayo yalionekana mazito.
Habari zilieleza kuwa JK alifanya hivyo kwa sababu siku zote amekuwa akitoa sapoti kubwa kwa wasanii wake wa Tanzania.
Baada ya Diamond kukutana na JK kwenye kikao hicho kizito na meneja
wa Trey Songz, Diamond aliandika kwenye kurasa zake za kijamii:
“Wapi utapata rais ambaye atakubali kutoa muda wake wa thamani ambao
unatafutwa karibu na kila mtu duniani…akautumia kukusaidia kukukutanisha
na kuku-connect na mdau mkubwa duniani katika tasnia uliyopo ili
kuhakikisha tu unafikia malengo na ndoto ya kazi zako….
“Dah! Asante sana mh. rais, Mwenyezi Mungu akuzidishie na kukusimamia katika uongozi wako na siku zote za maisha yako.”
Ijumaa lilifanya jitihada za kumpata Diamond live lakini jitihada zalikwama kutokana na maelezo kuwa bado alikuwa nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment