Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
HATIMA
ya Michael Richard Wambura kugombea au kutogombea Urais wa klabu ya
Simba SC itajulikana jioni ya leo, kufuatia jana kikao cha Kamati ya
Rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kumalizia kesi
yake.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya ameiambia BIN ZUBEIRY asubuhi ya
leo kwamba, jana walifanya kikao hadi Saa 4:30 usiku bila kumaliza na
wamepanga kukutana tena leo kuanzia Saa 6:00 mchana kuendelea.
“Lakini
tumefikia sehemu nzuri, tumewahoji pande zote mbili za wahusika wa
rufaa, kwa maana ya mkata rufaa na wakatiwa rufaa. Leo tutaanzia kwenye
kupitia maelezo yao na kisha kutoa maamuzi,” amesema Lugaziya, mmoja wa
mawakili wanaoheshimika nchini.
Kamati
ya Lugaziya ilikutana jana kuanzia Saa 5:00 asubuhi kwenye hoteli ya
Courtyard, Upanga, Dar es Salaam kusikiliza rufani moja inayopinga
uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba.
Michael
Wambura amewasilisha rufani yake TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya
Uchaguzi ya Simba iliyomwengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais
katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi
huu.
Hatima ya Michael Wambura (mwenye suti katikati) inaweza kujulikana leo jioni baada ya Kamati ya Rufani kuhitimisha zoezi la kupitia kesi yake |
No comments:
Post a Comment