Wanaumeee: Argentina wakishangilia baada ya kutinga fainali kwa ushindi wa penalti 4-2.
Messi kazini: Lionel Messi akijaribu kumtoka Nigel de Jong wakati wa mtanange huo.
Kiwango: Nahodha wa Uholanzi Robin van Persie akimiliki mpira dhidi wa wachezaji wa Argentina.
Hakatizi mtu: Mshambuliaji wa Uholanzi, Arjen Robben akifanyiwa madhambi na beki wa Argentina, Martin Demichelis.
Pozi: Mashabiki wa Argentina wakipozi kabla ya mtanange huo.
TIMU ya Argentina imetinga fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2014
baada ya kuiondoa Uholanzi kwa penalti 4-2 kwenye mchezo wa nusu
fainali uliopigwa Sao Paulo, Brazil usiku huu.
Kipa wa Argentina, Sergio Romero, alifanikiwa kuokoa mikwaju miwili
ya penalti iliyopigwa na Ron Vlaar na Wesley Sneijder wa Uholanzi baada
ya dakika 120 kumalizika timu hizo zikiwa suluhu.
Lionel Messi, Ezequiel Garay, Sergio Aguero na Maxi Rodriguez
waliifungia Argentina kwa penalti huku Waholanzi Arjen Robben, Dirk Kuyt
wakifunga penalti za Uholanzi.
Kwa matokeo ya leo, Argentina watamenyana na Ujerumani katika fainali
itakayopigwa Julai 13 mwaka huu huku Uholanzi na Brazil wakipepetana
kuwania nafasi ya mshindi wa tatu.
No comments:
Post a Comment